Bongo mpya inakuletea habari moto moto za kitaifa |kimataifa |michezo |burudani

Showing posts with label SPORTS. Show all posts
Showing posts with label SPORTS. Show all posts

Tuesday, 8 March 2016

Stori kamili ya Messi na Ronaldo walivyo sababisha kifo cha huyu jamaa



Image copyright
Image captionUbishi wa Messi na Ronaldo wasababisha mauti
Polisi nchini India wamemfungulia mashtaka ya mauaji mtu mmoja aliyemdunga kisu rafikiye waliyekosana kuhusu nani kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji bora duniani.
Raia huyo wa Nigeria alimdunga kisu mwezake vilevile mnigeria ambaye walikuwa wakibishana naye.
Inspekta mkuu wa polisi Kiran Kabadi ameiambia shirika la habari la AFP kuwa Michael Chukwuma, 21 ameshtakiwa kwa kuua katika mji wa Mumbai.
Yamkini yeye na mwenzake walianza gumzo kuhusu mchezaji bora katika kitongoji kimoja cha Nallasopara.
Chukwuma na wenzake walikuwa wamemtembelea marehemu kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.
Image copyrightGetty
Image captionRaia huyo wa Nigeria alimdunga kisu mwezake vilevile mnigeria ambaye walikuwa wakibishana naye.
''Mmoja wao alikuwa ni shabiki sugu wa mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Messi huku marehemu akimshabikia mfungaji mabao wa Ureno na Real Madrid Ronaldo''.
''Na kwa sababu ambayo haijulikani Chukwuma alimdunga marehemu mwenye umri wa miaka 34 kwa kisu na kumuua papo hapo.'' alisema Inspekta hyo wa Polisi.
Walioshuhudia wanasema kuwa marehemu alimrushia mshukiwa glasi usoni na mshukiwa akamshinda nguvu na kumdunga na ile glasi iliyovunjika, aliongezea Kabadi.

Tuesday, 5 January 2016

Mwaka unaanzaje kwa watani wa jadi!?

Friday, 1 January 2016

Van Gaal: Hakuna muujiza wa kuokoa Man Utd



Man UtdImage copyrightReuters
Image captionManchester United watakutana na Swansea Jumamosi
Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema hakuna muujiza wa kuimarisha hali ya klabu hiyo na lazima wahusika wote watie bidii.
United wamecheza mechi nane bila kushinda hata moja, sita zikiwa ligini, na kushuka hadi nambari sita.
Aidha, wameondolewa kutoka Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
“Hakuna muujiza, siri ni kuangalia yaliyotokea na kuona ni wapi tunaweza kujiboresha, kama timu na kama watu binafsi,” amesema, klabu hiyo ikijiandaa kukabili Swansea Jumamosi.
"Nimeshindwa mara tatu na Swansea, na baadaye unadadisi ni kwa nini ulishindwa. Mambo huwa hivyo, kisha unaendelea na mzunguko mwingine wa kufanya kazi.
"Unaweka mpango wa kulaza mpinzani wako na lazima ushawishi wachezaji wako. Baadaye, lazima ufanye mazoezi hadi uridhike. Kisha ujitolee na kujaribu kutekeleza mpango huo.
United walitoka sare 0-0 na Chelsea Jumatatu, mechi ambayo walionekana kucheza vyema baada yao kulazwa 2-0 na Stoke City siku ya Boxing Dei.
Image copyrightPA
Kabla ya mechi hiyo dhidi ya Chelsea, kulikuwa na wasiwasi kwamba huenda Van Gaal akafutwa baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya.
Alipoulizwa iwapo sare hiyo ilimpunguzia shinikizo, alisema: “Sijui kwa sababu shinikizo huwa kwako na wachezaji pia.”
United waliongoza ligi muda mfupi 21 Novemba baada ya kulaza Watford, mechi yao ya mwisho kushinda, lakini sasa wamo alama tisa nyuma ya viongozi Arsenal.
Van Gaal hata hivyo amewashukuru mashabiki kwa kuendelea kumuunga mkono.
"Hii si klabu yangu ya kwanza, labda itakuwa ya mwisho, ambapo nimepitia kipindi kibaya. Nimekuwa na vipindi vibaya na klabu zote nilizopitia na ninaweza kusema mashabiki hapa Manchester United ndio bora zaidi.
Van Gaal hata hivyo anaamini mwaka 2015 umekuwa mwema kwa klabu hiyo.

Friday, 25 December 2015

Rooney: man u wakaze buti meneja asifukuzwe



Van GaalImage copyrightReuters
Image captionVan Gaal amekabiliwa na shinikizo kutokana na klabu hiyo kutoandikisha matokeo mazuri
Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney amewashauri wachezaji wenzake kukaza buti ili kuokoa kibarua cha meneja wao Louis van Gaal.
Kufuatia kutoshinda katika Mechi 6 zilizopita na kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kibarua cha Van Gaal kimekuwa kwenye hatari kubwa.
Klabu hiyo imeporomoka hadi nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England na kujikuta wakiwa na Pointi 9 nyuma ya vinara Leicester City,
Rooney amenukuliwa akisema: "Hatujashinda katika wiki chache zilizopita na ni kawaida kupoteza kujiamini. Inabidi turejeshe imani kwani tuna michezo migumu na tunahitaji tuwe bora zaidi. Si kitu chema kufungwa kila mchezo. Ni ngumu kwa wachezaji. Tunaumia kwani sisi ni watu wa fahari na tunajionea fahari kuichezea Manchester United."

Sunday, 20 December 2015

ALIKIBA & CHRISTIAN BELLA_NAGHARAMIA.

Thursday, 17 December 2015

Jose Mourinho afutwa kazi Chelsea




MourinhoImage copyrightReuters
Image captionMourinho alikuwa tayari amekiri Chelsea hawawezi kumaliza katika nne bora ligini
Meneja wa klabu ya Chelsea ya Uingereza amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya.
The Blues walishinda Ligi ya Premia msimu uliopita lakini msimu huu mambo yamekuwa kinyume, na wamo alama moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja ligini.
Bodi ya klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatima ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich.
Klabu hiyo kupitia taarifa imesema mkataba kati ya klabu na meneja hiyo umekatishwa kwa maelewano kati ya pande zote mbili na ikamtakia kila la kheri Mourinho.
“Sifa zake Stamfrod Bridge na Uingereza zinajieleza na daima anakaribishwa kurejea Stamford Bridge,” klabu hiyo imesema kupitia taarifa.
“Sasa tutaangazia kuhakikisha kikosi chetu kilichojaa wachezaji wenye vipaji kinafikia uwezo wake. Hakutakuwa na taarifa zozote zaidi kutoka kwa klabu hadi kocha mpya ateuliwe.”
Mreno huyo mwenye umri wa miaka 52 amekuwa Chelsea kwa kipindi cha pili, kilichoanza Juni 2013.
Chelsea walimaliza alama nane mbele kileleni msimu uliopita na kutwaa taji pamoja na Kombe la Ligi lakini mwaka huu wameanza vibaya, wakishindwa mechi tisa kati ya 16 ligini kufikia sasa.
Mechi ya mwisho kwa Mourinho kwenye usukani ilikuwa Jumatatu walipochapwa na viongozi wa ligi Leicester City 2-1.
Mourinho alitia saini mkataba mpya wa miaka minne tarehe 7 Agosti mwaka huu na ndiye meneja aliyefanikiwa zaidi akiwa na Chelsea.
Alishinda mataji matatu ya Ligi ya Premia kipindi chake cha kwanza katika klabu hiyo kati ya 2004 na 2007.
Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos na miongoni mwa wanaopigiwa upatu kumrithi.

Tuesday, 15 December 2015

Mourinho avunja ukimya leo kuhusu chelsea



Image copyrightGetty
Image captionNaona aibu baada ya kushindwa tena
Siku moja baada ya kuambulia kichapo cha 2-1 dhidi ya Leicester City , mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho sasa anadai wachezaji wanamsaliti
Mourinho anasema wamefanya kila jitihada katika mazoezi kuhakikisha kuwa the blues wanaibuka videdea lakini wapi !
''Inachosha sana kutizama kazi ambayo tumefanya ikisalitiwa'' alisema Mourinho.
Image copyrightAFP
Image captionMourinho anasema wamefanya kila jitihada katika mazoezi kuhakikisha kuwa the blues wanaibuka videdea lakini wapi !
''Moja ya vipawa vyangu tajika ni uwezo wa kusoma na kuelewa mchezo kwa haraka,,hii ndio nahisi nimesalitiwa''
''Wakati mwengine nahisi kama vile nilijitahidi kuimarisha uwezo wa wachezaji wetu msimu uliopita na sasa inaonekana wameshindwa kustahimili ushindani katika kiwango hicho''alifoka Mourinho.
Msimu uliopita Chelsea walipoteza katika mechi tatu tu walizoshiriki lakini msimu huu, mambo yamewageuka na maji yamezidi unga.
Chelsea walipoteza mechi yao ya 9 msimu huu kati ya 16 walizocheza.
The Blues sasa wamejipata katika nafasi ya 16 wakiwa na alama moja tu zaidi ya timu zinazotishiwa kushushwa daraja msimu ujao.
Image copyrightReuters
Image captionThe Blues sasa wamejipata katika nafasi ya 16 wakiwa na alama moja tu zaidi ya timu zinazotishiwa kushushwa daraja msimu ujao.
Hata hivyo kinachomkera sana raia huyo wa Ureno ni kichapo cha 2-1 mikononi mwa vinara wa ligi kuu ya Uingereza Leicester City.
Mabao ya Jamie Vardy na Riyad Mahrez yaliisaidia 'The Foxes' katika uwanja wao wa nyumbani wa King Power Stadium.
Kinachowashangaza wapenzi wa timu hiyo ni kwanini wachezaji walioishinda ligi msimu uliopita sasa wanashindwa hata kustahimili ushindani kutoka kwa timu ndogo.
Iwapo motisha katika timu ya Chelsea haitaimarika kwa haraka kuna hofu kibarua cha mreno huyo kitaingia mchanga.
Kocha huyo wa Chelsea anakila sababu ya kuwa na hofu haswa wakijiandaa kukabiliana na Sunderland siku ya jumamosi.
Image copyrightGetty
Image captionKocha huyo wa Chelsea anakila sababu ya kuwa na hofu haswa wakijiandaa kukabiliana na Sunderland siku ya jumamosi.
Mourinho amekiri kuwa sasa haitawezekana kwa the Blues kufuzu kwa kinyang'anyiro cha kuwania kombe la mabingwa barani ulaya mwakani.
''Hatuwezi maliza katika nafasi 4 za kwanza ila tukijitahidi huenda tukacheza katika ligi ya Europa'' alisema Mourinho.
'Naona haya bila shaka'

Chelsea wachezea 2-1 kwa Leicester




ChelseaImage copyrightGetty
Image captionWachezaji wa Leicester City wakisherehekea ushindi dhidi ya Chelsea

Mabingwa watetezi wa ligi kuu England Chelsea wamezidi kutumbukia kwenye matatizo baada ya kupokezwa kichapo cha 2-1 na Leicester City.
Mshambuliaji wa Leicester Jamie Vardy ndie aliyeanza kupeleka msiba kwa The Blues baada ya kuandikisha bao la kwanza katika katika ya 34 ya mchezo. Winga Riyard Mahrez akaongeza bao la pili na la ushindi katika dakika ya 48 ya mchezo.
Bao pekee la kufutia machozi kwa upande wa Chelsea lilifungwa na Loic Remy aliyefunga kwa kichwa baada ya kupokea krosi nzuri kutoka kwa Pedro.
Kwa ushindi huu Leicester City wanarejea kileleni mwa ligi wakiwa na alama 35 baada ya kucheza michezo kumi na sita huku Chelsea wakijichimbia katika nafasi 16 wakiwa na alama 15 wakiwa wamepoteza michezo tisa katika michezo 16.
Mshambuliaji Jamei Vardy ameendelea kuongoza katika kinyang'anyiro cha mfungaji bora msimu huu akiwa sasa ametikisa nyavu mara 15 ligini msimu huu.

Monday, 14 December 2015

UEFA mzigo tayari


Baada ya kumalizika kwa hatua ya Makundi ya mechi za klabu Bingwa Ulaya UEFA, December 14 ndio siku ambayo droo ya kupanga ni timu zipi zitakutana katika hatua ya mtoano wa klabu Bingwa barani Ulaya. Jumla ya timu 16 ambazo zimefanikiwa kuingia hatua ya 16 zimeshajulikana toka December 9 ila December 14 ndio ilikuwa siku ya kufahamu ni timu zipi zitakutana,
2F3824FE00000578-3353037-image-a-25_1449700421460
Hizi ndio timu zilizofuzu hatua ya 16 bora.
Ratiba ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
  • Dynamo Kyiv vs Manchester City
  • Benfica vs Zenit
  • PSV vs Atletico Madrid
  • Juventus vs Bayern Munich
  • Arsenal vs Barcelona
  • PSG vs Chelsea
  • Roma vs Real Madrid
  • Gent vs Wolfsburg

Thursday, 3 December 2015

Barcelona yaichapa kipigo kikali Villanovense (Angalia magoli yote hapa)

Barcelona 6-1 Villanovense

liverpool yaendeleza vipigo Uingereza(Angalia magoli yote hapa)

Southampton 1-6 Liverpool

Sunday, 29 November 2015

Tazama magoli yote ya Barcelona vs Real sociedad hapa(video)

Thursday, 8 October 2015

Kamati yataka Blatter asimamishwe kazi



Image copyrightReuters
Image captionSepp Blatter
Kamati ya maadili katika shirikisho la soka duniani FIFA imependekeza Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA asimamishwe kazi kwa siku tisini.
Wanachama wa kamati hiyo walikutana wiki hii baada ya Jaji mkuu nchini Uswizi kufungua mashtaka ya uhalifu dhidi ya Blatter mwezi uliopita.
Blatter anatuhumiwa kwa kutia saini kandarasi zisizo na manufaa yoyote kwa FIFA mbali na kufanya 'malipo' kwa rais wa shirikisho la UEFA Michel Platini.
Blatter ambaye ni raia wa Uswizi amekuwa rais wa FIFA tangu mwaka 1998 na Platini ambaye anataka kumrithi amekana madai yoyote ya kufanya uovu.
Hakuna uamuzi ulioafikiwa kuhusu kumchukulia hatua yoyote Platini.

Monday, 5 October 2015

Wenger afurahia ushindi dhidi ya Man Utd



Arsene Wenger
Image copyrightAFP
Image captionWenger alikuwa ameshutumiwa kwa kumuacha nje kipa Petr Cech mechi waliyoshindwa na Olympiakos
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameeleza furaha yake baada ya klabu hiyo kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi Manchester United katika Ligi Kuu ya Uingereza Jumapili.
Wenger amesema alifurahishwa sana na uchezaji wa timu yake na kueleza kuwa walishangaza Manchester United kuanzia mwanzo wa mechi.
“Kuanzia kwa Petr Cech hadi kwa Theo Walcott wote walicheza vyema. Nimenoa timu nyingi kali lakini hakuna hata moja iliyoweza kucheza mechi 60 katika kiwango sawa. Lazima ukubali kwamba sisi ni binadamu,” alisema.
“Tuko kwenye kinyang’anyiro (cha kushindania taji), tuko alama mbili nyuma ya viongozi Manchester City na natumai matokeo ya leo yatatupa imani ya kuendelea kupigania taji.”
Arsenal walipata ushindi kupitia mabao mawili ya nyota wa Chile Alexis Sanchez na Mjerumani Mesut Ozil, mabao yote yakifungwa kipindi cha kwanza kwenye mechi hiyo iliyochezewa uwanja wa Emirates.
Kwa meneja wa Manchester United Louis Vvan Gaal, ilikuwa vigumu kukubali matokeo hayo.
„Tulianza vibaya sana, bila kuonyesha ari ya kushambulia na kutaka kushinda. Ilikuwa mara ya kwanza kwangu kushuhudia hilo katika timu yangu. Sikulitarajia hili,” amesema.
„Unapoipatia timu kama Arsenal mianya tele uwanjani ya kusakata gozi, basi unajua kwamba lazima utashindwa.”
Arsenal na Manchester United sasa zinatoshana alama ingawa Arsenal wako mbele wakishikilia nambari mbili kwenye jedwali kwa wingi wa mabao.
Timu hizo zitarudi mawindoni wiki mbili zijazo mnamo Oktoba 17, baada ya mapumziko ya wiki mbili ya mechi za kimataifa, ambako United watakutaka na Everton uwanjani Goodison Park nao Arsenal wawe ugenini Watford.

Brendan Rodgers afukuzwa Liverpool


Image copyrightAFP
Image captionBrendan Rodgers,afutwa kazi
Klabu ya soka ya Liverpool ya nchini Uingereza imemfukuza Meneja wake Brendan Rodgers baada ya matokeo mabaya ya muda mrefu.
Uamuzi wa kumfuta kazi Rodgers ulifanywa hata kabla ya mchezo ulioisha kwa suluhu dhidi ya Everton ambao uliwaacha Liverpool katika nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi ya England.
''Licha ya kuwa huu umekuwa ni uamuzi mgumu,tunaamini itatupa nguvu zaidi uwanjani,''ilisema taarifa ya klabu.
Meneja wa zamani wa klabu ya Chelsea na Real Madrid Carlo Ancelotti,kocha wa Ajax Frank de Boer na meneja wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund wamehusishwa kujiunga na klabu ya Liverpool katika siku za karibuni baada ya timu hiyo kuuanza msimu kwa kusua sua.

TP Mazembe kukutana na Alger fainali



Image captionTimu ya TP Mazembe
Klabu ya TP Mazembe ya Congo DRC, Itakutana na klabu ya Algeria USM Alger katika hatua ya fainali ya klabu bingwa barani Afrika.
Mazembe ilijihakikishia nafasi yake siku ya jumapili yaani jana baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya El Merrekh ya Sudan mjini Lubumbashi. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta alifunga mara mbili katika ushindi huo huku Muivarycoast Roger Assale akifunga goli la tatu.