Bongo mpya inakuletea habari moto moto za kitaifa |kimataifa |michezo |burudani

Showing posts with label NEWS. Show all posts
Showing posts with label NEWS. Show all posts

Tuesday, 15 March 2016

Vigogo wa Rahco watumbuliwa jipu Kortini




Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (Rahco), Benhadard Tito na wenzake wawili wamepadishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka manne.
Vigogo wawili wa Rahco na mfanyabiashara wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka, kula njama na kusababisha hasara ya dola za Marekani 527,540.
Mbali na Tito, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria wa Rahco, Emmanuel Massawe na mfanyabiashara ambaye pia ni mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma.
Washtakiwa hao watatu walisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, huku upande wa mashtaka ukiwa na Maghela Ndimbo, Janeth Machulya wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis.
 Mawakili hao, wakiongozwa na Vitalis walidai kuwa  washtakiwa wote watatu katika nyakati tofauti kati ya Septemba Mosi, 2014 na Septemba 30, 2015  katika Mkoa wa Dar es Salaam walikula njama ya kutenda makosa hayo chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.
Katika kesi hiyo, ilidaiwa kuwa Februari 27, 2015, Tito katika ofisi za Rahco zilizoko wilayani Ilala, alitumia madaraka yake vibaya kwa kuipitisha kampuni hiyo ya Rothschild kama mshauri wa mradi wa uimarishaji wa Reli ya Kati bila idhini ya Bodi ya zabuni ya Rahco, hivyo kwenda kinyume na Sheria ya Manunuzi ya Umma.
Tito na Massawe  wanadaiwa kuwa Machi 12, 2014 katika ofisi hizo za Rahco walitumia madaraka yao vibaya kwa kutia saini barua rasmi ya kuichagua kampuni hiyo, kama mshauri katika mchakato wa uimarishaji wa njia ya Reli ya Kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge).
Kati ya Machi 12 na Mei 20, 2015 katika ofisi za Rahco, Tito na Massawe wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kushindwa kuwasilisha mkataba wa huduma ya ushauri, baina ya kampuni hizo mbili kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Pia wanadaiwa kuwa kati ya Mei 20 na Juni 20, 2015 katika ofisi hizo washtakiwa hao, walishindwa kuwasilisha nakala ya mkataba kati ya kampuni hizo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Mbali na mashtaka hayo, washtakiwa hao kwa pamoja kwa nyakati tofauti kati ya Machi Mosi na Septemba 30, 2015 walitoa huduma ya ushauri kwa kampuni hiyo, bila kufuata taratibu za ununuzi na malipo na walisababisha hasara ya dola za Marekani 527,540 ambazo zililipwa kama  gharama za malipo ya awali.
Agosti 18, 2015, Tito akitekeleza majukumu yake, alitumia vibaya mamlaka kwa kuipatia kampuni ya China Railway Construction Corporation kazi ya ujenzi wa reli kwa kilomita mbili za kiwango cha kisasa kutoka Soga, iliyogharimu dola Marekani 2, 312,229.39 bila ya kuwa na  idhini ya bodi ya zabuni ya Rahco.
Washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.
Uamuzi wa dhamana utatolewa Ijumaa.

Hiki ndo kisa cha cha P Square kuvunjika


Baada ya kudumu kwa kipindi cha miaka 19, kundi la P-Square limevunjika rasmi. Hakuna aliyewahi kuwaza iwapo kundi hili maarufu na lililofanikiwa kuliko yote Afrika lingeweza kufika katika hatua hii.
Wizkid_Psquare_Afrobeat_promo-0127
Ni hatua iliyowashtua wengi. Kwa sasa Paul na Peter Okoye ni wasanii wawili wanaojitegemea. Paul aka Rudeboy ameanzisha record label yake, Rudeboy Records, na Peter aka Mr P ametangaza rasmi uongozi wake mpya.
Nini chanzo cha ugomvi wao?
Inaonekana kuwa ugomvi ndani ya kundi hili ulikuwepo kwa muda mrefu na kwa kiasi kikubwa ulitokana na kaka yao Jude, kuwa meneja wao. Peter alihisi uongozi wa kaka yake uliokuwa wa kifamilia zaidi ulikuwa hauko sawa na alihitaji mabadiliko.
“A manager is been employed by the artiste not the other way round. #truthBeTold,” aliandika Peter February 17 mwaka huu katika mfululizo wa tweets kuelezea matatizo yao.
“People change management and you r not different. Usher Raymond did it,BeyoncĂ© did it as well. So it’s not new. Peter and Paul have the right to sack the entire management team. Business is Business. #Period. Been nurturing and managing these problems for over 4yrs now. Don’t take my silence as a weakness. #done,” aliongeza.
Mwanzoni alipigania kundi lao lisife lakini uongozi ubadilike.
“What the fans want is Peter and Paul Psquare and that’s what I want. Period! Psquare is not breaking up. But the management needs to go.”
Lakini inaonekana kuwa Paul hakuwa tayari kumtoa kaka yao Jude kama meneja wao. Na hiyo ndiyo sababu Peter ameamua kujiondoa kwenye kundi hilo. Mapacha hao walijikuta wakigawanyika na kurushiana vijembe February 18 kwenye Instagram. Paul alipost picha ambayo awali ilikuwa ikiwaonesha wao na kaka yao Jude, lakini akamuondoa Peter na kuandika:
This is where I belong and this is where I stand…….you do music in the studio, not on social media, you have family issues, you discuss that in close doors, not on social media ….. Family is family, blood is blood …. If you don’t do family business, then who am I to you?”
Kitendo hicho kilimuumiza Peter aliyejibu: And cutting me off from a picture and replacing me with a studio set says it all my bro. All because you want to sound matured and letting the pple insult and Laff at me. Peter Okoye the social media rant. I wish you well in all you do my bro. God bless our hustle.”
Mama yao angekuwepo yasingetokea?
Paul anaamini kama mama yake angelikuwa hai, yote yanayoendelea yasingetokea.
“Wish you were around, now I understand what these life is without having a mother, you’ve played your part thank you very much mum, miss you,” aliandika Paul kwenye picha ya marehemu mama yao aliyoiweka Instagram.
Mashabiki wameuamia lakini inabidi waukubali ukweli kuwa kundi hilo lililoiteka Afrika kwa kishindo kwa takriban miongo miwili limevunjika. Na sasa Peter na Paul wanaanza maisha ya solo huku Peter tayari akiwa ameanza kufanya show zake mwenyewe. Nani atafanya vizuri zaidi ya mwenzake? Muda utaongea.

Kagame kumuiga Rais Magufuli

mawaziri
Image copyrightAFP
Image captionRais Kagame amesema ziara nyingi zinazofanywa na mawaziri EAC hazina umuhimu
Rais wa Rwanda Paul Kagame amelaumu Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutumia pesa ‘kiholela’ kutokana na mawaziri kufanya ziara za mara kwa mara kuhudhuria mikutano.
Amesema mawaziri wa nchi yake wanatumia chombo hicho kama njia ya kujinufaisha kwa kufanya ziara na kuhudhuria mikutano ya jumuiya hiyo isiyo muhimu.
Ameahidi kuiga mfano wa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kutokomeza ufisadi huo wa kusitisha ziara za mawaziri alizotaja kuwa za kufuja mali ya taifa.
Akiongea katika mkutano wa faragha wa viongozi wa taasisi zote za serikali nchini Rwanda, Rais Kagame amesema suala la ufisadi nchini humo linachukua mwelekeo mpya na kasi ya ajabu na kwamba hawezi kuendelea kuvumilia.
Rais Kagame aidha amesema Jumuiya ya Afrika Mashariki imeanza kuwa ghali na mzigo kwa taifa lake akisema mawaziri katika mataifa wanachama wanatumia jumuiya hiyo kama chombo cha kuchota pesa kwa kubuni mikutano ya kila siku baadhi akiitaja kuwa haina umuhimu wowote.
Amesema mawaziri wake wasiopungua watano wanasafiri kama mara tatu kwa wiki kushiriki mikutano ya EAC popote inapotokea katika nchi wanachama na kwamba ziara hizo zinaigharimu serikali kitita kikubwa cha pesa.
“Ni kama mawaziri wa nchi hizi walikubaliana kushinikiza serikali zao kuwa lazima wahudhurie kila aina ya vikao vya jumuia hii kwa kisingizio kuwa waziri anayeshindwa kuhudhuria nchi yake inachukuliwa hatua ama inaonekana kupinga juhudi na mikakati ya jumuiya,” amesema Rais Kagame.
Moja ya njia alizosema anaweza kutumia ni kumpa waziri wake wa masuala ya EAC Valentine Rugwabiza jukumu la kushughulikia masuala yote yanayohusu jumuiya hiyo.
MagufuliImage copyrightStatehouse Tanzania
Image captionRais Magufuli amepunguza ziara za maafisa wa serikali nje ya nchi
Amepongeza juhudi za Rais wa Tanzania John Magufuli za kukomesha ufisadi uliokuwa umekithiri katika taasisi za serikali, akisema lazima na yeye afuate nyayo za Rais Magufuli katika suala zima la kukomesha ufisadi na ufujaji wa mali ya serikali.
Rwanda inaorodheshwa ya kwanza katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kupambana na rushwa na ufisadi.
Mwandishi wa BBC Yves Bucyana anasema miaka ya nyuma viongozi kadhaa wa wilaya na taasisi nyingine za serikali walipoteza kazi zao na kutupwa jela kwa makosa ya kuhusika na rushwa na ufisadi.

Rais Magufuli amalizana na Rais wa kampuni ya Total


Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Javier Rielo amemuhakikishia Rais wa Magufuli kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha Mafuta kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga Tanzania haraka iwezekanavyo kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.
r3
Javier Rielo ametoa ahadi hiyo tarehe 14 March 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli Ikulu Dar es salaam ambapo imefahamika mradi huo utahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo litasafirisha mafuta ghafi mapipa 200,000 kwa siku kutoka ziwa Albert Uganda hadi bandari ya Tanga na utarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.
R1Katika Mazungumzo hayo Javier amemueleza Rais Magufuli kuwa Kampuni yake inatarajia kutumia dola za kimarekani karibu bilioni 4 ambazo tayari zimeshaandaliwa ambapo pamoja na kuukaribisha uwekezaji huo mkubwa kwa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka kampuni hiyo kuharakisha mchakato wa kuanza kwa mradi, na ameshauri muda wa miaka mitatu uliopangwa kuukamilisha mradi huo upunguzwe ili manufaa yake yaanze kupatikana mapema.
r2
Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, amesema Wizara yake ipo tayari kuhakikisha mradi huo unafanikiwa na itatoa ushirikiano wa kutosha kuharakisha utekelezaji wake.
Prof. Mhongo amebainisha kuwa licha ya kwamba hali ya kijiografia, hali ya hewa na bandari ya Tanga vinatoa mazingira bora ya kufanikiwa kwa mradi huo, Tanzania pia inatarajia kunufaika na bomba hilo, kwa kuwa kuna tafiti mbili za mafuta zinazoendelea katika ziwa Tanganyika na ziwa Eyasi, ambazo zikikamilika kwa mafanikio inatarajiwa bomba hilo litasaidia kusafirisha mafuta yake.
r4

Diamond kumtambulisha msanii mpya leo wasafi

Baada ya label ya WCB kumsaini mkali wa hit single ya Bado ‘Harmonize’ na kuendelea kufanya vizuri kwenye soko la muziki wa Tanzania.
Sasa good news nyingine iliyotolewa na staa Diamond Platnumz  ambaye ni msimamizi wa label hiyo alisema kwamba leo March 15 watatangaza msanii mpya waliemsaini katika label yao.
Kupitia kwenye ukurasa wa twitter aliwataarifu mashabiki kwa kuandika..’Panapo Majaaliwa Jumatano Hii Wcb_Wasafi tutamtambulisha rasmi Kijana Mwingine Mpya…tafadhali wadau tunaomba sana Support zenu’>> Diamond

Hapa ninayo interview ya Harmonize ambaye ni msanii wa kwanza kusainiwa katika label ya WCB akizungumza jinsi alivyokutana na Diamond Platnumz

Wema afunguka kuhusu penzi lake na Pedeshee wa Kikongo



Tangu mwaka 2016 uanze miongoni mwa story zilizochukua headlines kwenye mitandao mbalimbali ni hii inayomuhusu mwigizaji staa wa Tanzania, Wema Sepetu kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na Mcongo.
Sasa leo kupitia instagram amejibu tetesi hizo na kuandika..‘Sijawahi na sitowahi kuwa na mwanaume Mcongo wa aina yoyote ile… Sasa nashangaa watu wameona mimi ndo daraja la kuwapa umaarufu… Im Tired… Huyo apocalypse sijui kitu gani aint my man… I only know him as a friend.So please guys niacheni kidogo tafadhal… Alam-siq…!!!🙏🏽🙏🏽🙏🏽And ontop of all dat I think u all know me by now nikiwa na mtu sijivungi kumtangaza maana huwa I live to please my heart… Mwanaume wangu nadhani anajulikana’>> @wemasepetu
‘Sasa endeleeni kumpa huyo baba attention sababu yeye nako naona kashaona ni kamchezo kakupatia followers.Na nyie mnampa airtime ya kutosha anaendelea Ananiudhi na mimi kiukweli hadi napata hasira.But nakaa tu kimya… This is too much now’>>> wemasepetu

Monday, 14 March 2016

P Square yapasuka

Kundi la P-Square halipo tena. Member wa kundi hilo, Peter Okoye amejitenga na kuanzisha management yake.
927562_198845507152036_2113012156_n
Hatua hiyo imekuja baada ya muimbaji huyo kutofautiana na meneja wao, Jude Okoye ambaye ni kaka yake. Jude anaendelea kuwa meneja wa pacha mwingine, Paul. Kupitia Instagram, Peter ameandika:

Work Mood. Thanks for all the love, support and concern pls continue to remain blessed as always. For bookings and enquiries, please contact my new management on 08037531340 [email] bookmrp2@gmail.com ||oyesng@yahoo.com #MrP.
Wakati huo huo Paul ambaye ameanzisha record label yake, Rudeboy Records, amepost picha ya mama yao na kuandika:
Wish you were around, now I understand what these life is without having a mother, you’ve played your part thank you very much mum, miss you.”

Wakazi wa Kigoma wagomea ujenzi wa bandari Kavu


Jeshi la Polisi Kigoma,limelazimika kutumia nguvu na mabomu ya machozi kuwatawanya mamia ya wakazi wa mtaa wa katosho na kahabwa kata ya kibirizi katika manispaa ya Kigoma ujiji ,waliokuwa wakiandamana kupinga nyumba zao kuwekwa notisi ya kuhama kupisha ujenzi wa bandari kavu.


Majina ya wakuu wa mikoa haya hapa


Image copyrightStatehouse Tanzania
Image captionRaisiMagufuli awateua wakuu 13 wapya wa mikoa
Rais Magufuli amewateua wakuu 13 wapya wa mikoa miongoni mwa orodha mpya ya wakuu 26 wa mikoa iliyotangazwa leo na ikulu ya rais.
Rais John Pombe Magufuli amewahifadhi wakuu 13 waliohudumu katika serikali ya Jakaya Kikwete.
Uteuzi huo umetangazwa na katibu mkuu kiongozi, Mussa Ibrahim Iyombe.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari iliyotiwa sahihi na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, katika ikulu, Gerson Msigwa, Viongozi hao wote walioteuliwa wataapishwa katika hafla maalum itakayoandaliwa jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa tatu asubuhi jijini Dar es salaam.
Orodha ya wakuu wa mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
Majina ya Wakuu wa Mikoa
Paul MakondaDar es Salaam
Ezekiel Elias KyungaGeita
Salum Mustafa KijuuKagera
Raphael MuhugaKatavi
Emmanuel MagangaKigoma
Godfrey ZambiLindi
Dkt. Steven KebweMorogoro
Zerote StevenRukwa
Anna Malecela KilangoShinyanga
Methew MtigumweSingida
Antony MatakaSimiyu
Aggrey MwanriTabora
Martine ShigelaTanga
Jordan Mungire RugimbanaDodoma
Said Meck SadickKilimanjaro
Magesa MulongoMara
Amos Gabriel MakallaMbeya
John Vianey MongellaMwanza
Daudi Felix NtibendaArusha
Amina Juma MasenzaIringa
Joel Nkaya BenderaManyara
Halima Omary DendeguMtwara
Dkt. Rehema NchimbiNjombe
Evarist NdikiloPwani
Said Thabit MwambunguRuvuma
Chiku GalawaSongwe (Mkoa mpya)

Tuesday, 8 March 2016

Ombeni Sefue afunguka juu ya kusimamishwa kazi


Baada ya kudumu Ikulu kwa takribani siku 127 zikiwamo 67 tangu aongezewe muda wa mwaka moja akiwa na Serikali ya Awamu ya Tano, Balozi Ombeni Sefue ameshukuru heshima aliyopewa na Rais John Magufuli kwa muda wote aliomsaidia kutekeleza majukumu yake ya ukatibu mkuu kiongozi na kueleza kuwa Serikali ya sasa ni ya mabadiliko. 

Wakati Sefue akiondoka, mhandisi John Kijazi amepokea kijiti cha ukuu wa utumishi serikalini na kuahidi kuwa atafuatilia mazingira ya watumishi wote pamoja na mazingira yao, ili kurekebisha panapohitajika kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na tija kwa wananchi.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa kwa mrithi wake, licha ya kumshukuru Rais, Balozi Sefue aliwataka watendaji wote serikalini kumpa ushirikiano wa kutosha Balozi Kijazi ili kuleta ufanisi kwenye huduma za umma.

Namshukuru Rais kwa kuniamini kwa kipindi chote nilichodumu naye. Ni heshima kubwa kuwatumikia Watanzania pamoja naye. Nitampa ushirikiano wowote atakaouhitaji katibu mkuu kiongozi mpya kwenye utekelezaji wa majukumu yake,” alisema Sefue.

Rais Magufuli, ameahidi na mara zote amekuwa akisisitiza adhma yake ya kutumbua majipu kwa watumishi wote ambao hawaendani na kasi yake.

Tangu taarifa za mabadilio hayo zilipotangazwa jana, kumekuwepo na tetesi nyingi kuwa huenda Sefue naye ni jipu lilikuwepo ikulu, suala ambalo halikupata maelezo ya kutosha kutoka kwa balozi huyo.

Alipoulizwa juu ya tetesi hizo alijibu kwa ufupi: “Hii ni Serikali ya mabadiliko.”

Kwa upande wake Kijazi, alisema atafanya kazi kwa kuzingatia vipaumbele vya Rais huku akimshauri namna sahihi za kuboresha mazingira ya utumishi serikalini.

Sunday, 6 March 2016

Rais Magufuli amemteua Katibu mkuu kiongozi mpya

Rais John Pombe Magufuli amemteua Balozi Mhandisi John Kijazi kuwa Katibu mkuu Kiongozi hivyo Balozi Ombeni Sefue Atapangiwa Kazi nyingine.

Trump na Cruz ngoma droo


Image copyrightGetty
Image captionTrump na Cruz watoshana nguvu
Wagombea wakuu,katika kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu wa Marekani,kwenye chama cha Republican wameshinda majimbo mawaili kila mmoja katika kura ya mchujo ya hivi karibuni.
SenetaTed Cruz ameshinda majimbo ya Kansas na Maine huku bwenyenye Donald Trump, akitwaa majimbo ya Louisiana na Kentucky.
Trump tayari ameshashinda majimbo mengine kadhaa ya awali na anaongoza wapinzani wake katika Republican, jambo linalowatia wasiwasi mkubwa vigogo wa chama hicho ambao wamefadhaisha na sera tata na za uchokozi anazoziendeleza Trump, wengi wakisema zinakwenda kinyume na maadili ya Marekani.
Sasa Cruz anasema yeye ndiye anaweza kuwa mgombea mbadala wa billionaire huyo wa New York Trump.
Image copyrightGetty
Image captionTrump na Cruz wanawataka wagombea wenza wajiondoe iliwakabiliane moja kwa moja
Kwa upande wa chama cha Democratic bi Hillary Clinton ameshinda Louisiana,huku mpinzani wake senator Bernie Sanders akishinda Kansas na Nebraska.
Akihutubia wapinzani wake amesema demokrasia ya Marekani haipaswi kuharibiwa na mabillionare.