Caitlyn Jenner, ambaye kabla ya kubadili jina alikuwa akifahamika kama Bruce Jenner ambaye baba wa kambo wa Kim Kardashian aliyejibadilisha na kuwa mwanamke, amevunja rekodi ya dunia kwa kuwa mtu wa kwanza kufikisha followers milioni moja wa Twitter ndani ya saa nne na dakika tatu.
Caitlyn alitweet furaha yake kupitia akaunti yake mpya ya Twitter.
Rekodi hiyo hapo awali iliwekwa na rais wa Marekani, Barack Obama baada ya kufungua akaunti yake binafsi ya Twitter mwezi uliopita.
Caitlyn Jenner
Mnamo mwezi Aprili Bruce Jenner alijibadilisha maumbile katika mahojiano na Diane Sawyer wa ABC.
Mnamo mwezi Mei Jenner mwenye umri wa miaka 65 alijadiliana na familia yake kuhusu hatua yake ya kujibadili maumbile katika kipindi cha ''keeping up with the Kardashians''.
Sasa Jenner yuko tayari kujitangaza kama Caitlyn kwa ulimwengu.
Caitlyn Jenner
Katika picha iliopgwa na Annie Leibovitz,picha ya mwanariadha huyo wa zamani ilichapishwa katika jarida la Vanity na ndani ya gazeti hilo ,jenner anaweka wazi maumbile yake mapya.
Baada ya kupata wafuasi zaidi ya milioni moja kwa mda wa saa nne ,Caitlyn Jenner amevunja rekodi ya mtandao wa twitter kulingana na rekodi za dunia za Guiness.Amemshinda Barrack Obama aliyeshikilia taji hilo kwa wiki mbili.
0 comments:
Post a Comment