Mgombea urais ACT-Wazalendo kupatikana Agosti 10.

Posted by Unknown on 11:31 with No comments

Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.
Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kuwa mgombea wa kiti cha urais kupitia chama hicho atafahamika rasmi ifikapo Agosti 10, mwaka huu huku chama hicho pia kikitoa taratibu, ratiba na vigezo vya mgombea wa kiti hicho kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.
Aidha vikao vya kujadili na kupitisha wagombea kupitia kamati ya uongozi wa jimbo na kamati ya uongozi wa mkoa vitakaa kuanzia Julai 27 hadi Agosti 3 huku kamati kuu na halmashauri kuu itakaa Agosti 8 na 9, kabla ya mkutano mkuu wa taifa kumpitisha mgombea huyo, Agosti 10 mwaka huu.
Hayo yalisemwa jana katika mkutano wa hadhara mkoani hapa na Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na kusema kuwa katika mkutano maalumu uliofanyika mkoani Tabora juzi Jumamosi, pamoja na mambo mengine, Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho, kilipokea, kilijadili na kupitisha taratibu na sifa kwa wagombea nafasi ya urais.
 
Alisema Halmashauri Kuu imepitisha taratibu na vigezo na kwamba mwanachama anayetaka kugombea nafasi ya urais atachukua fomu kwa Sh. 100,000, mgombea wa ubunge ni Sh. 20,000 na udiwani ni Sh. 10,000.
 
Aliongeza kwamba mwanachama anayetaka kugombea nafasi ya urais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar atajaza fomu kwa katibu mkuu wa chama hicho kuanzia Julai Mosi na kurudisha fomu Julai 29, mwaka huu.
 
Kabwe alisema kuwa kamati ya Uadilifu itawachambua wagombea wote wa nafasi ya urais na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu kupitia Sekretariati ya Chama.
 
"Kamati Kuu itakuwa na jukumu la kupendekeza wagombea wa nafasi ya urais kwa Halmashauri Kuu kwa vigezo, sifa na alama mbalimbali kwa kila mgombea aliyejitokeza," alisema Kabwe.
 
Kwa upande wa sifa za wagombea wote wa nafasi ya urais, Kabwe alisema watapaswa kukidhi vigezo na sifa za kiongozi wa ACT-Wazalendo kama zilivyoanishwa katika Nyongeza ya Kwanza ya Katiba, Sehemu ya III na Sehemu ya IV. 
 
Alisema sifa hizo zitakwenda pamoja na vigezo na sifa za kikatiba zilizoanishwa katika sehemu ya Katiba ya chama hicho pamoja na Katiba ya nchi.
 
Chama cha ACT-Wazalendo kimeendelea na ziara yake na leo kitafanya mikutano mjini Bukoba, Kagera.Na Christina Mwakangale, Geita
 
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema kuwa mgombea wa kiti cha urais kupitia chama hicho atafahamika rasmi ifikapo Agosti 10, mwaka huu huku chama hicho pia kikitoa taratibu, ratiba na vigezo vya mgombea wa kiti hicho kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar. Aidha vikao vya kujadili na kupitisha wagombea kupitia kamati ya uongozi wa jimbo na kamati ya uongozi wa mkoa vitakaa kuanzia Julai 27 hadi Agosti 3 huku kamati kuu na halmashauri kuu itakaa Agosti 8 na 9, kabla ya mkutano mkuu wa taifa kumpitisha mgombea huyo, Agosti 10 mwaka huu.
 
Hayo yalisemwa jana katika mkutano wa hadhara mkoani hapa na Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na kusema kuwa katika mkutano maalumu uliofanyika mkoani Tabora juzi Jumamosi, pamoja na mambo mengine, Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho, kilipokea, kilijadili na kupitisha taratibu na sifa kwa wagombea nafasi ya urais.
 
Alisema Halmashauri Kuu imepitisha taratibu na vigezo na kwamba mwanachama anayetaka kugombea nafasi ya urais atachukua fomu kwa Sh. 100,000, mgombea wa ubunge ni Sh. 20,000 na udiwani ni Sh. 10,000.
 
Aliongeza kwamba mwanachama anayetaka kugombea nafasi ya urais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar atajaza fomu kwa katibu mkuu wa chama hicho kuanzia Julai Mosi na kurudisha fomu Julai 29, mwaka huu.
 
Kabwe alisema kuwa kamati ya Uadilifu itawachambua wagombea wote wa nafasi ya urais na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu kupitia Sekretariati ya Chama.
 
"Kamati Kuu itakuwa na jukumu la kupendekeza wagombea wa nafasi ya urais kwa Halmashauri Kuu kwa vigezo, sifa na alama mbalimbali kwa kila mgombea aliyejitokeza," alisema Kabwe.
 
Kwa upande wa sifa za wagombea wote wa nafasi ya urais, Kabwe alisema watapaswa kukidhi vigezo na sifa za kiongozi wa ACT-Wazalendo kama zilivyoanishwa katika Nyongeza ya Kwanza ya Katiba, Sehemu ya III na Sehemu ya IV. 
 
Alisema sifa hizo zitakwenda pamoja na vigezo na sifa za kikatiba zilizoanishwa katika sehemu ya Katiba ya chama hicho pamoja na Katiba ya nchi.
 
Chama cha ACT-Wazalendo kimeendelea na ziara yake na leo kitafanya mikutano mjini Bukoba, Kagera.
Categories: