Mlipuko wa bomu wawaua watu 23 Nigeria
Posted by Unknown on 19:09 with No comments
Mshirikishe mwenzako

Watu 23 wameuawa Kaskazini mwa Nigeria wakati mabomu yaliyokuwa yameachwa nyuma na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram yalipolipuka katika kambi yao ya zamani.
Wapiganaji wa kiraia wanaosaidiana na Serikali kupambana na Boko Haram walikuwa wakipekua kambi hiyo iliyokuwa imehamwa na wapiganaji wa Boko Haram karibu na mji wa Monguno wakati milipuko ilipotokea.
Inadaiwa kuwa watu hao walikuwa wakisherehekea
baada ya kupata mabomu hayo wakati ambapo bomu moja lililipuka na kusababisha madhara hayo makubwa.
Tukio hilo linaonyesha baadhi ya matatizo ambayo raia wanaendelea kukabiliana nayo hata wakati Boko Haram wanapoendelea kutimuliwa.
habari kutoka bbc swahili
http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/06/150617_nigeria-bomu
Categories: NEWS
0 comments:
Post a Comment