Mpiganaji wa Kiislam Mokhtar auawa Libya
Posted by Unknown on 10:50 with No comments

Serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa imesema mashambulio ya Marekani ya anga nchini Libya, yamemuua mpiganaji mwandamizi wa Kiislam, Mokhtar Belmokhtar.
Wizara ya ulinzi ya Marekani imethibitisha kuwa Belmokhtar alikuwa mlengwa wa mashambulio hayo ya Jumamosi, lakini imesema bado inafanya tathmini ya matokeo ya operesheni hiyo.
Mokhtar Belmokhtar mzaliwa wa Algeria anaamini kuamuru kufanyika kwa shambulio baya katika mtambo wa gesi nchini Algeria miaka miwili iliyopita ambapo wafanyakazi 38 wa mtambo huo waliuawa-- wengi wao wakiwa wageni waliuawa.
Kifo cha Belmokhtar kimekuwa kikiripotiwa mara nyingi katika siku zilizopita, lakini baadaye kubainika kuwa si habari za kweli.
Categories: NEWS
0 comments:
Post a Comment