Watalii 8 'walisababisha' tetemeko la ardhi

Posted by Unknown on 14:54 with No comments

Mlima Kinabalu
Raia wanne wa kigeni wamefikishwa mahakamani nchini Malaysia kwa kusababisha tetemeko la ardhi.
Raia hao wa kigeni wanatuhumiwa kujipiga picha wakiwa uchi juu ya mlima mrefu zaidi nchini humo jambo lililowakasirisha miungu wao waliosababisha tetemeko hilo lililotimia vipimo vya 5.9 kwenye vipimo vya Richter.

Watalii wakiokolewa katika mlima Kinabalu baada ya tetemeko la ardhi
Kisa hicho kimefanyika kabla ya tetemeko la ardhi kutokea katika mlima huo wa, Kinabalu na kuwauwa wakweaji milima kumi na nane.
Baadhi ya raia wa eneo hilo wanalaumu janga hilo la tetemeko la ardhi kwa matendo ya raia hao ambao wameshtumiwa kutoheshimu mila na tamaduni za wageni hususan kwasababu mlima huo ni mtakatifu.
Maafisa wa serikali wangali wanawatafuta watu wengine 6 wanaokabiliwa na tuhuma zizo hizo.
Bendera ya Malaysia ikipaa karibu na mlima Kinabalu
Miongoni mwa wale ambao tayari wamefikisha mahakamani ni mwanamke mmoja mwingereza na raia wengine wawili kutoka Canada na mmoja mholanzi.
Mlima Kinabalu wenye kina cha futi elfu kumi na tatu ni maarufu sana miongoni mwa watalii.
Categories: