Kiongozi wa waasi BURUNDI asema wanajiandaa kumuondoa NKURUZINZA

Posted by Unknown on 16:49 with No comments
JENERALI, LEONARD NGENDAKUMANA
Afisa wa ngazi za juu katika jeshi la  BURUNDI, aliyekuwa ni miongoni mwa walioongoza mapinduzi  ya kijeshi yaliyokwama  nchini humo mwezi  MEI mwaka huu, JENERALI, LEONARD NGENDAKUMANA, amesema bado kundi lake linajiandaa kumwondoa madarakani Rais PIERRE NKRUNZIZA wa  nchi hiyo.
Jenerali NGENDAKUMANA amesema dhamira ya kumwondoa madarakani Rais NKRUNZINZA bado ipo pale pale  kutokana na  kiongozi huyo kuiingiza BURUNDI kwenye machafuko baada ya uamuzi wake wa kuwania tena kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu kinyume cha katiba.
Vyama vya upinzani nchini BURUNDI vimepinga hatua ya NKRUNZINZA kuiongoza tena nchi hiyo.
Categories: