Mapigano mapya yaripotiwa Yemen
Posted by Unknown on 16:36 with No comments

Kuna ripoti za mapigano mapya nchini Yemen muda mfupi baada ya usitishwaji mapigano wa saa sita kuanza kutekelezwa.
Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa muungano unaongozwa na Saudi Arabia uliendesha mashambulizi ya angani mjini Sanaa na mji ulio Kusini Magharabi wa Taiz.
Mapema baraza la usalama la umoja wa mataifa lilitoa wito kwa pande zote nchini Yemen kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano.
Mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu yana matumaini ya kusafirisha misaada baada ya miezi kadha ya mapigano kati ya serikali inayoungwa mkono na Saudi Arabia na waasi wa Houthi.
Categories: NEWS
0 comments:
Post a Comment