Marekebisho ya Ugiriki 'yatafeli'
Posted by Unknown on 17:01 with No comments

Harakati za kulikwamua taifa la Ugiriki katika madeni yake zimekosolewa na mawaziri ambao wamefutwa kazi kwa kupinga mpango huo.
Aliyekuwa waziri wa fedha Yanis Varoufakis ameiambia BBC kwamba mpango huo ni janga na kwamba waziri mkuu mwenyewe hauamini.
Bwana Varoufakis alijiuzulu saa kadhaa baada Ugiriki kupiga kura ya kupinga marekebisho ya sheria yaliopendekezwa katika kura ya maoni.
Mawaziri waliopinga masharti ya makubaliano mapya waliondolewa katika serikali siku ya ijumaa.
Bwana Varoufakis alijiunga na zaidi ya robo ya wabunge wa Syriza kupinga masharti hayo mapya.
Categories: NEWS
0 comments:
Post a Comment