Wagombea urais CCM watambulishwa visiwani Zanzibar

Posted by Unknown on 09:00 with No comments

Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. JOHN MAGUFULI ameahidi kushirikiana na viongozi wengine wa kuhakikisha wanachochea
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa kwenye gari la wazi pamoja na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan kwenye mitaa ya Michenzani Zanzibar.
Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. JOHN MAGUFULI ameahidi kushirikiana na viongozi wengine wa kuhakikisha wanachochea maendeleo kwa wananchi.
Dr.MAGUFULI ameyasema hayo katika viwanja vya ofisi ya CCM KISIWANDUI ZANZIBAR katika Mkutano maalum wa kutambulishwa kwa wananchi baada ya kuchaguliwa na Mkutano Mkuu wa CCM kwa ajili ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA

Awali akizungumza katika Mkutano huo, Mgombea Mwenza wa Urais SAMIA SULUHU HASSAN amewataka wanawake nchini kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Wagombea hao kupitia CCM wametambulishwa kisiwani UNGUJA ikiwa ni Mkutano wa tatu baada ya ile iliyofanyika DODOMA na DSM
Categories: