Chile yapigwa na tetemeko

Posted by Unknown on 09:34 with No comments



Image copyrightAFP
Image captionwanawake wakiwa katika hali ya sintofahamu mjini Santiago
Tetemeko kubwa la ardhi limeipiga Chile na kusababisha tishio la kutokea kwa tsunami, katika eneo lake la pwani na maeneo mengine ya bahari ya Pacific.
Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 8.3 katika vipimo vya ritcha, lilipiga maeneo ya pwani na kuenea kwa kilomita 250 kaskazini magharibi wa mji mkuu Santiago.
Nchi hiyo imewahamisha wakazi milioni moja katika eneo la pwani, Rais wa Chile amethbitisha watu watano wamepoteza maisha baada ya tetemeko hilo kupiga
Kumeshuhudiwa matetemeko mingine midogomidogo katika eneo hilo
Categories: