M/kiti CWT aingia matatani kwa kuhudhuria mkutano wa Lowassa
Posted by Unknown on 09:26 with No comments


Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Chato mkoani Geita, ameshtakiwa kwa kosa la kwenda kuhudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.
Serikali imemfungulia mashtaka Mwenyekiti huyo, Lucas Michael maarufu Masai kwa madai ya kukiuka maadili na utaratibu wa utumishi wa umma.
Michael ameshtakiwa kwenye Tume ya Utumishi wa Umma, Idara ya Utumishi wa Walimu wilayani hapa.
Michael anadaiwa siku ya mkutano huo wa kampeni, alimweleza mgombea huyo kuwa serikali imeshindwa kuwasafirisha walimu waliostaafu kurudi makwao, kulipa madai ya walimu na kutowapandishwa madaraja.
Pia, alidai kusikitishwa na kitendo cha uongozi wa Wilaya ya Chato kuwaandama baadhi ya walimu wanaoonekana kuunga mkono upinzani na wanaoiunga mkono CCM hawachukuliwi hatua yoyote ya kinidhamu.
Mwenyekiti huyo wa CWT alihudhuria mkutano wa kampeni za mgombea huyo alipofika wilayani Chato Septemba 19, baada ya kupokea mwaliko wa Chadema Wilaya ya Chato akiwa kama mdau wa elimu.
Kwa mujibu wa mashtaka hayo, Michael anadaiwa kukiuka maadili na utaratibu wa utumishi, Kanuni namba 65(1) na kutakiwa kujieleza.
.
Categories: NEWS
0 comments:
Post a Comment