Athari za video za ngono katika mahusiano
Posted by Unknown on 13:48 with No comments
Nilikuwa nasoma makala kwenye gazeti moja nikakutana na habari ya mtu huyu ambaye ameathirika na kitendo cha kutazama picha za ngono na tendo la kufanya punyeto tokea akiwa shule ya sekondari.

Akaendelea kusema kwa sasa amekuwa kwenye ndoa kwa miaka mitatu lakini tatizo hilo linaendelea ingawa mke wake hajui jambo hilo linavyomsumbua. Kinachotokea ni kwamba anapokuwa peke yake ndani ya nyumba peke yake huangalia picha hizo na kuanza kupiga punyeto, ingawa alidhani angeacha mara tu baada ya kuoa.
Athari alizopata kwa kuendekeza tabia hizo ni kukosa hamu kufanya tendo la ndoa na mkewe wakati mwingine hivyo kuna wakati anapata ugomvi na mkwewe akidhani kwamba anakwenda nje ya ndoa. Aliandika habari yake ili aweze kupatiwa msaada namna gani ya kuondokana na tatizo hilo. Kutokana na mtaalamu huyo ambaye anashauri watu ambao wameangukia kwenye tatizo hilo ni kwamba tabia hizo zinaweza kukuharibia ndoa yako kabisa kama uko miongoni wa waathirika.
Hakuna jambo ambalo unaweza kuliacha kirahisi kama umezoea kufanya kwa muda mrefu, kubadili tabia mbaya kunahitaji nguvu ya ziada kujitoa na wewe mwenyewe kutumia juhudi kubwa kuhakikisha unaacha kabisa.
Tabia ya kuangalia picha za ngono ni mbaya na inakubidi kuacha kabisa, ingawa kuna watu wanaiona kama si tatizo kama umeona inakuletea shinda kwenye ndoa ujue ni tatizo wala hakuna namna nyingine ambayo unaweza kutetea jambo hilo.
Si rahisi kuacha ila unahitaji kutumia muda mwingi ukiwa na mkeo vilevile kujadili jambo hilo kwa pamoja ili kupata msaada kutoka kwake. Vile vile unahitaji kuepuka kukaa peke yako bila kazi yoyote ya msingi ndani ya nyumba ili kufuta mawazo ya kufanya punyeto au kuangalia picha za ngono.
Jadili na mkeo ili muweze kupata suluhisho la kudumu, mjulishe kwamba umekuwa na shida hiyo ili kuokoa ndoa yako ingawa unahitaji lugha nzuri ya kuleta mada hiyo mezani. Mke anaweza kukusaidia kutatua suala hilo kihisia na kimwili na kwamba anahitaji kuwa na wewe kwa ukaribu zaidi ingawa juhudi kubwa inakubidi wewe mwenyewe kudhamiria kwa dhati kabisa kuondokana na tabia hiyo mbaya.

Categories: DID YOU KNOW?
0 comments:
Post a Comment