‘Ufyatulianaji mkali’ wa risasi unaendelea Paris

Posted by Unknown on 08:57 with No comments


Image copyrightReuters
Image captionPolisi wamezingira eneo la Place Jean Jaures mtaa wa Saint Denis
Ufyatulianaji mkali wa risasi umetokea kaskazini mwa Paris katika mtaa wa Saint Denis na ripoti zinasema operesheni ya polisi kuhusiana na mashambulio ya Ijumaa inaendelea.
Duru za polisi zinasema kumekuwa na ufyatulianaji wa risasi.
Awali, duru za kiusalama zilisema video ya kiusalama ilikuwa imeonyesha huenda kulikuwa na mshambuliaji wa tisa mashambulio hayo ya Ijumaa.
Watu 129 walifariki kwenye mashambulio yaliyotokea maeneo sita mjini Paris.
Kundi la Islamic State (IS) limesema ndilo lililotekeleza mashambulio hayo.
Ripoti moja inasema barabara zimefungwa eneo la Place Jean Jaures mtaa wa Saint Denis.
Uwanja wa taifa wa michezo wa Stade de France, ambako washambuliaji walilipua mabomu Ijumaa, umo kwenye mtaa huo.
Categories: