Arusha yateketea kwa mafuriko

Posted by Unknown on 15:32 with No comments



Arusha. Watu watatu wamefariki dunia huku familia zaidi ya 70 zikikosa mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa na mafuriko yaliyotokana na mvua za vuli zinazoendelea kunyesha huko wilayani Arumeru, mkoani Arusha.
Hata hivyo, mifugo 150 wakiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo imepotea kutokana na maafa hayo.
Akizungumza leo, mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Vijijini, wilayani Arumeru, Fidelis Lumato amesema mvua hizo zimeleta maafa hayo katika kata nane za halmashauri hiyo baada ya kunyesha usiku wa kuamkia leo.
Kutokana na maafa hayo, Lumato amewataka wakazi wote wanaoishi mabondeni kuhamia sehemu zilizoinuka kwani huenda mvua za masika zikaleta maafa zaidi.
Familia nyingine zimehamishiwa shuleni huku uongozi ukiendelea kutafuta mahali salama  pa kuishi kwa waathirika wa mvua hizo.

Categories: