India yachukua hatua juu ya mapenzi ya jinsia moja.

Posted by Unknown on 22:56 with No comments


Image copyrightAFP
Image captionMji wa kaskazini mwa India, Aligarh, umepiga marufuku filamu mpya ya wapenzi wa jinsia moja
Mji wa kaskazini mwa India, Aligarh, umepiga marufuku filamu mpya yenye jina la mji huo, kuoneshwa huko, kwa sababu inahusu mapenzi ya jinsia moja.
Meya wa mji huo Shakuntala Bharti, alisema jina la filamu linafaa kubadilishwa, kwa sababu linahusisha mji huo na mapenzi ya jinsia moja, na hivo, kama alivosema, inautusi mji.
Chama cha wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Waislamu mjini huimo, wamekariri maoni yake.
Filamu hiyo inahusu maisha ya profesa wa chuo kikuu, ambaye alisimamishwa kazi, kwa sababu alifanya mapenzi ya jinsia moja, na baadaye alijiuwa.
Aliyetengeneza filamu hiyo, Hansal Mehta, amesema malalamiko yanayofanywa ni "chuki dhidi ya wapenzi wa jinsia moja".
Categories: