Magufuli ana kwa ana na marais Afrika Mashariki.

Posted by Unknown on 09:38 with No comments
Rais John Magufuli akisalimiana na Mbunge wa
Rais John Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Daudi Ntibenda.
Arusha. Rais John Magufuli, amewasili jijini Arusha jana, kushiriki mkutano wa 17 wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki, utakaofanyika Machi 2.
Katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine, wakuu hao ambao nchi zao ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), watajadili kuhusu hati za pamoja za kusafiria, ombi la nchi za Sudan Kusini na Somalia kutaka kuwa wanachama na udhibiti wa magari chakavu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustino Mahiga alisema maandalizi yote muhimu ya mkutano huo yamekamilika.
Alisema Machi mosi, Rais anatarajiwa kuanza kupokea marais wengine wa Afrika ya Mashariki kwa ajili ya mkutano huo na baadaye Machi tatu, kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Arusha- Holili ambayo ni sehemu za barabara za kisasa za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Mambo watakayojadili
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa kitengo cha habari cha habari cha jumuiya hiyo Richard Owora, baadhi ya ajenda za mkutano ni kupokea taarifa ya baraza la mawaziri kuhusiana na masuala ya jumuiya hiyo, kulinda viwanda vya nguo na viatu vya ndani na kuzindua mfumo wa sekta binafsi katika jumuiya ya Afrika ya mashariki.
JPM awashukuru wananchi
Akizungumza baada ya kushuka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) akitokea jijini Dar es Salaam,Rais Magufuli aliwashukuru wananchi waliojitokeza kumpokea.
Aidha, aliwataka wananchi hao kuendelea kujitokeza kuwapokea marais wengine wa nchi za Afrika ya Mashariki, ambao wanatarajia kuwasili jijini hapa kuanzia kesho.
Alitumia fursa hiyo kuwapongeza wanachama wa CCM kukamilisha salama uchaguzi wa CCM wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wanachama waliohamia Chadema

Categories: