Dk Sezibera amsifia Magufuli.

Posted by Unknown on 13:12 with No comments
Katibu Mkuu Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
Katibu Mkuu Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayemaliza muda wake, Dk Richard Sezibera akizungumza kwenye mkutano mkuu wa nne wa EAC uliofanyika Dar es Salaam juzi. Picha na Venance Nestory 

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametajwa kuwa nembo mpya ya uongozi barani Afrika. Sambamba na hilo, rushwa na ufisadi vimebainishwa kuwa chanzo cha maendeleo duni katika nchi za Afrika Mashariki.
Hayo yalisemwa juzi na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayemaliza muda wake, Dk Richard Sezibera wakati wa ufunguzi wa mkutano wa jukwaa la wadau na wajasiriamali wa nchi za Afrika Mashariki.
Katika mkutano huo unaodhaminiwa na Kampuni ya Trademark East Africa, katibu huyo alisema hayo ndiyo mambo yanayoathiri dhana ya utawala bora.
Aliongeza kuwa wananchi huchagua watu wasio na maadili ili wawe viongozi wao, kwa kuwa tayari wanakuwa wamepokea rushwa na zawadi mbalimbali wakati wa kampeni.
“Naona ndiyo maana viongozi hao hurudisha fadhila ya ufisadi,” alisema.
Alimtaja Rais Magufuli kuwa mmoja wa viongozi wanaoonyesha dalili ya kupiga vita rushwa na ufisadi kwa manufaa ya wananchi na kwamba, ni vyema viongozi wengine wakaiga mfano huo ili kutimiza dhana ya utawala bora.
Mkurugenzi wa Trademark East Africa, Jason Kap-Kirwok alisema nchi wanachama wa EAC zitapewa mafunzo hadi pale zitakapofuata misingi ya utawala bora.
“Ni vyema kuwawezesha wananchi kifikra na uwezo, ili wafanikiwe yote hayo hutokana na viongozi wao kufuata utaratibu wa uongozi bora unaofuata Katiba kwa ajili ya kuwatumika vyema,” alisema Kap-Kirwok.

Categories: