Chanjo ya Malaria yaonesha mafanikio Kenya
Posted by Unknown on 10:27 with No comments
Chanjo ya Malaria yaonesha mafanikio Kenya
Majaribio ya chanjo dhidi ya malaria nchini Kenya yameonesha
dalili nzuri ya mafanikio.
Wanasayansi watafiti kutoka Chuo kikuu cha Oxford Uingereza
wamesajili asili mia 67% ya mafanikio katika majaribio ya chanjo hiyo kwa
wakenya 121.
Utafiti huo ni wa pili wa haiba yake katika kipindi cha
miongo miwili iliyopita.
WHO inasema kuwa visa milioni 198 vya malaria viliripotiwa
mwaka wa 2013 huku takriban watoto 584,000 wakipoteza maisha yao.
Majaribio ya chanjo nyengine tofauti pia yameonesha
mafanikio katika kuwakinga watoto wachanga.
Takwimu zinaonesha kuwa watoto 1,300 wanakufa kila siku
chini ya jangwa la Sahara kutokana na ugonjwa huo.
Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa visa milioni 198
vya malaria viliripotiwa mwaka wa 2013 huku takriban watoto 584,000 wakipoteza
maisha yao.
Ajabu ni kuwa hakujakuwa na mafanikio makubwa kuhusu mbinu
za kupambana na kirusi kinachosababisha malaria.
Virusi vya Malaria
''Plasmodium falciparum'' anayeishi katika mbu
walioambukizwa.
Kimsingi watafiti hao wamegundua kuwepo kwa aina nne ya
virusi.
Aidha haijabainika iwapo chanjo hiyo itakabiliana na aina
zote nne za virusi.
Utafiti huo ambao umekuwa ukiwafuatilia wanaume 121 kwa
majuma 8 umegundua kuwa idadi ya virusi vinapungua kwa thuluthi mbili.
Mbu aliyeambukizwa na virusi vya ''Plasmodium falciparum''
Watafiti hao wamegundua aina ya chanjo inayovamia kirusi
ndani ya maini ya mgonjwa.
''Kiwango cha juu cha mafanikio kama tulivyoshuhudia hapa ni
ishara nzuri ''.
''Tunachohitaji ni utafiti zaidi ili tuwanusuru mamilioni ya
watoto wanaoathirika na Malaria''
Alisema Mtafiti mkuu Prof Adrian Hill.
Kimsingi watafiti hao wamegundua kuwepo kwa aina nne ya
virusi.
Hatua ya pili ya utafiti huu sasa unaelekea Burkina Faso
ambapo utafiti utahusisha watoto.
Profesa Chris Drakeley, kwa upande wake alionya kuwa
kunahaja kubwa ya tahadhari maanake huenda madawa haya yakafaa watu wazima
ilhali watoto ndio wanaoathirika kwa kiwango kikubwa zaidi.
Hata hivyo Profesa Drakeley, anashauri kinga dhidi ya
ugonjwa huu ni kulala ndani ya vyandarua vilivyotibiwa.
habari kutoka bbc swahili
Categories: NEWS
0 comments:
Post a Comment