Mfumo mbovu wa uteuzi chanzo cha matatizo CCM
Posted by Unknown on 17:15 with No comments
BAADHI ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wameulalamikia mfumo wa uteuzi ndani ya chama hicho na kudai kuwa ni mbovu na umekisababishia chama hicho kujikuta katika matatizo.
Hali hiyo inadaiwa kuwafanya wanachama wengi kuhamia katika vyama vingine vya viasa ambavyo ni vya upinzani wakiwemo viongozi wa juu wa chama hicho.
Madai hayo yanakuja wakati ambapo chama hicho kimeingia katika kampeni zake za kuelekea uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani baada ya kukamilisha baadhi ya taratibu za uchaguzi mkuu.
Mgombea udiwani, Oneasmo Nywage katika kata ya Pandambili (CCM) akikiri uwepo wa mapungufu kwa baadhi ya wanachama licha ya chama hicho kujiwekea sera na taratibu nzuri.
Naye katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wilaya ya Kongwa, Monica Nyabu yeye anataja baadhi ya masuala ya kupewa kipaumbele pindi uongozi mpya utakapoanza kazi baada ya uchaguzi mkuu.
Categories: NEWS
0 comments:
Post a Comment