JE KAMA ASSET ZA DK SLAA ZINGE MLIDHISHA AU ANGE KUWA MGOMBEA URAISI WA UKAWA ANGE YASEMA HAYA?

Posted by Unknown on 20:30 with No comments


 Kwa tuhuma alizotoa Dk Slaa kuhusu Lowassa, kama katibu wa chama cha CHADEMA wa kipindi hicho. hakupaswa hata kufikiria kuhusu vitu alivyo viita ASSET au LIABILITY, kwa maneno mengine FAIDA au HASARA, kwasababu huwezi kusema kwamba kujua mchango atakao uleta katika chama ndo kumfanye msafi na kama anamtuhumu Lowassa hivo.
 Je huu ni mda muafaka kuyasema hayo?  kwa mtazamo wangu Hapana, kwa kua mwnye Dk Slaa ametuambia fika kuwa lengo la kuyasema haya ni kutaka kuwaelimisha wananchi, Dk Slaa kama katibu wa CHADEMA ange yasema haya mwanzoni kabisa, pale Lowassa alipomba kujiunga na CHADEMA ili wananchi wangemuelewa vizuri Lowassa vile anavyo mjua yeye.
 Je kuingia kwa Lowassa kuna fanya CHADEMA kuwa cha mafisadi? pia ni hapana, kwa kuwa sidhani muumini mmoja au hata wengi wakienda kwa mchungaji kanisani au kwa sheikh msikitini, kutafanya watu wengine wote msikitini au kanisani wawe waovu kwa kua tunaamini hizo ni sehemu za wokovu na kumjua Mungu hivyo hao watu lazima watabadilika.
 Je Dk Slaa nae ni Kapi? jibu ni ndio kwakuwa makapi yanatoka CCM na kwenda CHADEMA na sababu ya yeye na wale wanaotoka CCM sahivi wote inafana, hawakulidhishwa na utendaji wa chama hicho.
 Je unafikiri ni kwanini Dk Slaa ameamua kuyasema haya sahivi?








Categories: