Makosa ya barabarani sasa kulipwa kielektroniki
Posted by Unknown on 07:56 with No comments
Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Kampuni ya Max Malipo wamezindua kifaa kipya cha kielektoniki cha kufanyia malipo kwa madereva wa magari waliovunja sheria za usalama barabarani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga alisema hicho kifaa kitaanza rasmi kutumika kesho kwa Jiji la Dar es Salaam kwa majaribio.
“Hii imetokana na malalamiko kutoka kwa wamiliki wa magari na madereva kwamba wamekuwa wakilipishwa faini na askari wa barabarani pasipo kupewa risiti halali ya serikali.” Aliema Kamanda Mpinga
Aliongeza kuwa kifaa hicho kitakuwa kinagundua endapo gari ni bovu, au dereva amevunja sheria kama vile kutovaa mkanda au kwenda kwa mwendokasi, hivyo taarifa zote zitachukuliwa pamoja na namba ya gari na kuhifadhiwa, na dereva aliyefanya kosa hawezi kukataa kwa sababu ataonyeshwa taarifa zote zilizokusanywa.
“Ulipaji huu wa kielektroniki hauna utofauti sana na ule unaotumika kulipia bili za umeme, maji na ada za magari kwa njia ya mtandao na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),” alisema.
Alibainisha kwamba huduma hii mpya itamuwezesha mmiliki wa gari endapo amemuazimisha mtu gari lake kugundua kama gari lake limekamatwa na kutozwa pesa.
Kamanda Mpinga alisema dereva aliyebainika na kosa anatakiwa alipe ndani ya siku saba, na zaidi ya siku saba atatozwa asilimia 25 ya tozo la awali na baada ya siku 14 na kuendelea atatozwa ziada ya asilimia 50 ya tozo la awali.
Categories: NEWS
0 comments:
Post a Comment