Mfumuko wa bei za bidhaa wang’ang’ana

Posted by Unknown on 08:45 with No comments
Mkurugenzi wa Sensa za Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo (kushoto) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mfumuko wa bei.
Mkurugenzi wa Sensa za Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo (kushoto) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mfumuko wa bei.
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa taarifa juu ya mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali nchini kwa mwezi Agosti, 2015 pamoja na mwenendo wa mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki. 
Mkurugenzi wa Sensa za Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo amesema hali ya mfumuko wa bei kubaki asilimia 6.4 inamaana kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma unaenda kwa kulingana na mwaka 2014.

Kwesigabo amesema wastani wa bei zimeongezeka kutoka 158.81 kwa mwaka 2015 hadi 149.31 Agosti mwaka jana. Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Agosti, 2015 umepungua hadi asilimia 10.2 kutoka asilimia 10.6 ilivyokuwa mwezi Julai, 2015.
Amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa mwezi Agosti, 2015 kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi hiki.
Bei za mavazi ya wanaume zimeongezeka 5.9%, mavazi ya wanawake 3.7%, kodi ya pango 5.3%, mkaa 2.4%, mazulia 4.3%, vifaa vya nyumbani vya malazi 3.1%, madawa 12.7%, huduma za kuona madaktari 4.3%, pamoja na huduma za malazi kwa 3.5%.
Hata hivyo mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi umeongezeka asilimia 0.02 ikilinganishwa na 0.14% ilivyokuwa mwezi Julai, 2015. Takwimu za bei zimeongezeka hadi 158.81 mwezi Agost, 2015 kutoka 158.78 mwezi Julai, 2015.
Aidha amesema baadhi ya bei za bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na gesi kwa 2.0%, mafuta ya taa kwa 2.3%, mazulia kwa 1.4, dizeli kwa 3.8% pamoja na petrol kwa 8.3%.
Kwesigabo amesema uwezo wa Tsh. 100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia Tsh. 62 na senti 97 mwezi Agosti, 2015 kutoka mwezi Septemba, 2010 ikilinganishwa na Tsh. 62 na senti 98 ilivyokuwa mwezi Julai, 2015.
Kwa upande wa hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki unakaribiana na Tanzania, ambapo mfumuko wa bei mwezi Agosti, 2015 nchini Kenya umefikia 5.84% kutoka 6.62% mwezi Julai, 2015 na Uganda umefikia 4.80% kutoka 5.4% mwezi Julai, 2015
Categories: