Ushindi wa 69% kwenye uchaguzi mkuu 2015 CCM.
Posted by Unknown on 23:02 with No comments
Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Dk.John Pombe Magufuli.
CHAMA cha Mapinduzi CCM kimesema kina uhakika wa kushida kwa asilimia 69 katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, January Makamba amesema kwa utafiti wa kisayansi ambao umefanywa na taasisi huru umebainisha kuwa chama hicho tawala kina uhakika wa kutetea kiti cha urais.
“Kamati ya kampeni ya Kitaifa ilitoa kazi hii kwa kampuni huru na kuonyesha kuwa tutashinda kwa asilimia 69. Huu ni utafiti wa kisayansi, hatuna shaka na ushindi. Upepo upo upande wetu,” anasema mwanasiasa huyo.
Aidha, mwanasiasa huyo amesema mgombea wa urais wa CCM, Dk. John Magufuli ameonyesha uimara katika kampeni kwani kwa sasa anafanya mikutano 10 kwa siku akitumia gari.
Kwa upande mwingine, CCM imesema uchaguzi ni tukio la kupita hivyo ni vema kipaumbele kiwekwe kwenye umoja wa kitaifa na kuachana na siasa zinazoweza kuwagawa Watanzania kikanda, kikabila na hata kidini.
Katika mkutano huo pia Makamba ambaye ni mjumbe wa kamati ya kampeni za urais za Dk Magufuli, alipinga hoja iliyotolewa na Ukawa kuwa mdahalo uliopangwa kufanywa na Twaweza uwashirikishe wenyeviti wa vyama pekee.
Makamba alisema popote pale duniani, midahalo inawahusisha wagombea wa nafasi husika na si vinginevyo.
Categories: NEWS
0 comments:
Post a Comment