Tabora yaangamia kwa ushirikina.
Posted by Unknown on 17:14 with No comments
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athumani alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akizungumza na viongozi wa madhehebu ya dini, vyama vya siasa, wazee na maofisa wa polisi mjini Tabora.
Alisema Wilaya ya Kaliua inaongoza mkoani hapa kwa kuwa na watu 84 waliouawa ikilinganishwa na nyingine.
Alisema licha ya Mkoa kuwa na idadi kubwa ya matukio ya mauaji pia ni wa 11 nchini kwa uhalifu wa aina mbalimbali ikiwamo unyang’anyi, ujambazi, uporaji wa kutumia silaha na matumizi ya dawa za kulevya.
“Tutachukua hatua za kisheria kwa wote watakaoendelea kujihusisha na matukio ya uhalifu, mauaji na rushwa ikiwa ni pamoja na kuwasaka wote wanaomiliki silaha kinyume na taratibu,” alisema Athumani.
Pia, aliwataka askari na maofisa wake kuacha tabia ya kukumbatia wahalifu, kuomba na kupokea rushwa.
Askofu Paul Meivukie wa Kanisa la TAG Tabora, aliitaka Serikali kuweka mikakati itakayosaidia kupunguza mauaji hayo.
“Hali hii inasikitisha sana, watu 300 wanaweza kujaza kanisa kubwa la hapa mjini na watu 84 waliouawa wilayani Kaliua ni sawa na waumini wa kanisa au msikiti wa wilaya, hivyo ni bora tukaangalia namna bora ya kuunda kikosi kazi cha kutoa elimu ya kufichua wahalifu,” alisema Askofu Meivukie. Sheikh Hussein Nkumilwa alisema wakati mwingine mauaji hayo husababishwa na vitendo vya rushwa vilivyokithiri kwa baadhi ya watumishi wa umma.
Categories: habari
0 comments:
Post a Comment