Usafiri MV Serengeti kuanza Jumatano.
Posted by Unknown on 17:16 with No comments
MV Serengeti ilisitisha safari zake tangu Februari 15, baada ya kupata hitilafu katika injini ya kulia ilipokuwa ikisafiri kutoka Mwanza kwenda Bukoba.
Meli hiyo ililazimika kurejea Mwanza bila kupakia abiria wala mizigo ili kuepuka madhara kwa kuwa ilikuwa ikitumia injini moja.
Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Mkoa wa Mwanza, Mwassa Winton alisema jana kuwa matengenezo ya meli hiyo yatakamilika Machi 9.
“Matengenezo yalichelewa kidogo kutokana na vipuli kuchelewa kufika Mwanza. Hivi sasa tumeshapata vipuli na mafundi wanaendelea na kazi usiku na mchana,” alisema Winton.
Wafanyabiashara wa ndizi, Leokadia Thobias na Fabiani Kaijage walisema biashara yao imeathirika kwa sababu wanalazimika kusafirisha mizigo kwa kutumia magari au meli maboti madogo kwa gharama kubwa ikilinganishwa na ile ya meli.
Naye Christina Mshomi aliyekutwa akinunua ndizi katika soko kuu jijini Mwanza alisema wanauziwa mkungu mmoja kwa kati ya Sh25,000 hadi Sh35,000 kutoka Sh15,000 hadi Sh20,000 wakati meli ilipokuwa inafanya kazi.
Mkazi wa Mwanza, Rutahiwa Ijumba aliiomba Serikali kununua meli mpya badala ya kutumia mamilioni ya fedha kukarabati zilizopo.
Categories: habari
0 comments:
Post a Comment