RIO FERDINAND ASTAAFU SOKA
Posted by Unknown on 18:20 with No comments
Rio Ferdinand, 36 beki wa zamani wa Manchester United na timu ya Taifa ya England ametangaza kustaafu soka.
Rio ametangaza kustaafu soka baada ya klabu ya
Queens Park Rangers kutangaza kumtema kwenye kikosi chake. Alisema hayo katika mahojiano na BT Sport, na aliandika ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter kuwashukuru waliomtakia kila la heri baada ya kifo cha mkewe Rebecca ambaye wamezaa naye watoto watatu.Rio Ferdinand akiwa na marehemu mkewe Rebecca
Ferdinand alimpa sifa kocha wake wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kwamba ni mfano wa kuigwa kutokana na ujuzi wake.
July 2002 Rio alikuwa beki ghali katika historia ya soka ya Uingereza wakati akisajiliwa kutoka Leeds United kwenda Manchester United kwa pauni milioni 30.
Categories: SPORTS
0 comments:
Post a Comment