DIAMOND AKIRI KUWA AY NDIYE CHANZO CHA MAFANIKIO YAKE

Posted by Unknown on 09:38 with No comments
AY The Legend of Music in Tanzania, tunaweza sema ni baba wa muziki wa bongo flava, amesaidia sana katika kuupeleka muziki wa Tanzania nje ya nchi bila kusahau kuwasaidia wasanii wengi kutambulika kimataifa kama Ommy dimpoz, Diamond n.k

Katika ujumbe wake wa kumpongeza AY kwenye siku yake ya kuzaliwa Jumapili hii, Diamond amedai kuwa AY ndiye aliyemuunganisha na Davido hadi wakafanya remix ya wimbo wake ‘Number One’ uliobadilisha maisha yake.

“Misingi na Daraja Imara la kimataifa ulio tujengea na unayozidi kutujengea ndio leo inatusaidia vijana wako nasi kuweza kupenyeza na kutangaza kazi zetu kimataifa,” ameandika Diamond kwenye Instagram.
“Pengine watu hawajui kuwa wewe ndio uliyeniwezeshea kufanikisha Collabo langu na Davido, Kuniunga na Godfather na vingi ambavyo naamini ndio Mwanzo wa safari yangu ya Kimataifa… Nakuheshim sana Brother, na daima nitahakikisha sikuangushiemoji…Happy birthday Bro.”
Categories: