NEC kutangaza majimbo mapya..

Posted by Unknown on 09:37 with No comments

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva.
Tume ya Taifa Uchaguzi (Nec), imesema kuwa inatarajia kutangaza majimbo mapya ndani wiki hii.
 
Akizungumza na NIPASHE jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, alisema maandalizi ya kugawanya majimbo yamekamilika.
 
“Tunatarajia kutangaza majimbo hayo mapya ndani ya siku mbili au tatu wiki hii, kila kitu kimeshakamilika hivyo tusubiri ndani ya muda huo,” alisema Jaji Lubuva.
 
Mei mwaka huu Nec ilitangaza kugawa majimbo na kusema imezingatia vigezo mbalimbali ikiwamo idadi ya watu, upatikanaji wa mawasiliano hali ya kijiografia na vigezo vingine kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa rais na wabunge za mwaka 2010.
 
Jaji Lubuva alisema ugawaji wa majimbo hufanyika kila baada ya miaka 10 na ugawaji huo utafanyika kabla ya Oktoba kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu katika majimbo na kuona kuna umuhimu wa kugawa majimbo.
 
Wakati Nec ikiahidi kutangaza mgawanyo wa majimbo, wiki hii wadau katika maeneo kadhaa nchini kupitia kamati za ushauri za mikoa na wilaya wamekuwa wakipendekezo kuanzishwa kwa majimbo mapya.
 
Kwa upande wake, vyama vya upinzani vinavyoundwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Jumatatu wiki hii viliitupia lawama Nec kwamba kuchelewa kutangaza mgawo wa majimbo na mipaka ya kata kumewaathiri wachelewe kugawanya majimbo. Ukawa inaundwa na Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.
 
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) Jumatatu wiki hii ilitangaza mgawo wa majimbo ya Zanzibar kwa kuongeza majimbo manne upande wa Unguja na kuongeza idadi ya majimbo visiwani kuwa 54 kutoka 50 ya awal
Categories: