Udiwani, ubunge kwa Lowassa kigugumizi
Posted by Unknown on 17:21 with No comments
.jpg)
Uchukuaji wa fomu bado mambo magumu
Kamati ya Siasa ya CCM yabana maamuzi
Akizungumza baada ya kikao hicho, alisema wajumbe wamejadili masuala kadhaa lakini yapo ya ndani ambayo yanahitaji utekelezaji.
Katika hali inayoonyesha kupata kigugumizi, Kimaro alikataa kuyataja mambo hayo akisema hayapaswi kutangazwa.
“Tumekutana na kujadili mambo mengi kwa kina, tumefikia muafaka lakini yapo mambo ambayo bado yanahitaji utekelezaji, haya ni mambo ya ndani tunayafanyia utekelezaji,” alisema.
Hata hivyo, alisema wajumbe wote 16 wa kamati hiyo wamekubaliana kuendelea kuwahamasisha wanachama kuchukua fomu za kugombea nafasi za udiwani na ubunge kabla ya Julai 19, mwaka huu, saa 10 jioni, siku ambayo ni ya mwisho kuchukua fomu na kuzirejesha.
Alisema kazi ya kuwahamasisha wanachama imeanza kuzaa matunda baada ya wanachama watatu zaidi kujitokeza na kuchukua fomu za kuwania ubunge ambapo sasa wamefikia wanachama wanne.
Aliwataja waliochukua fomu hizo kuwa ni Sakaya Kabuti, Mwalimu Lorinyo Mkoti na Loata Sanare ambao walichukua jana, wakati Mbayani Tayayi yeye alichukua fomu yake siku ya Jumatano wiki hii.
Kuhusu waliochukua fomu kwa upande wa udiwani, alisema idadi yao imeanza kuongezeka ikilinganishwa na ile ya juzi ambayo ilikuwa ni wanachama watatu tu toka kata tatu. Aliwataja waliokwishachukua fomu ni kutoka kata za Mswakini, Lepurko na Engutoto.
Jimbo la Monduli lina kata 20 ambazo ni Engaruka, Engutoto, Esilalei, Lepurko, Loksale, Majengo, Makunyuni, Meserani, Nalalani, Lemooti, Moita, Monduli Juu, Monduli Mjini, Mfereji, Mswakinji, Mto wa Mbu, Migungani, Selela, Sepeko na Lashani.
Alisema ni azma ya chama chake kusimamisha mgombea katika kila kata, hivyo jukumu lake ni kuhakikisha wagombea wanapatikana.
Hata hivyo, alisema kata zote tayari zimekwishapata wagombea isipokuwa Kata ya Monduli Mjini ambayo bado wanachama hawajajitokeza kuomba fomu za kuwania udiwani lakini uhamasishaji unaendelea.
Alitaja idadi ya wanachama waliochukua fomu katika kata hizo na idadi yake kwenye mabano kuwa ni Majengo (1), Mto wa Mbu (1), Migungani (3), Makuyuni (1), Engutoto (2), Monduli Juu (3), Mfereji (2), Moita (1), Meserani (2), Loksale (2), Esilalei (1) Selela (1), Lepurko (2), Engaruka (2), Mswakini (1), Lemoti (1), Sepeko (1) na Nalalani (1).
Akizungumza na NIPASHE juzi, Kimaro alisema kumekuwa na kasi ndogo ya wanachama kuomba nafasi za udiwani na ubunge hali ambayo alisema inatokana na kusuasua kwa wanachama hao baada ya kukatwa kwa jina la Mbunge wao Edward Lowassa, katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM Julai 12, mwaka huu.
Alisema kufuatia kukatwa kwa Lowassa katika kinyang’anyiro hicho, kumekuwa na propaganda nyingi katika mitandao ya kijamii, na zingine toka kwa baadhi ya madiwani wa zamani ambao wanawahamasisha wanachama kutochukua fomu za kuomba nafasi hizo wakitaka wasubiri kwanza kauli kuhusu hatma ya mbunge wao.
Categories: NEWS
0 comments:
Post a Comment