VANESSA MDEE APATA SHAVU NIGERIA
Posted by Unknown on 17:10 with No comments

Vanessa Mdee akihojiwa kwenye studio za Trace Nigeria
Vanessa Mdee yupo nchini Nigeria anakoendelea na ziara kwenye vyombo mbalimbali jijini Lagos.
Tayari ameshazunguka na kuhojiwa kwenye vituo vyote vikubwa vya redio na TV nchini humo kupromote single yake ‘Nobody But Me.’
Akiwa huko Vee Money ameshirikishwa kwenye wimbo wa msanii Shaydee utakaotoka hivi karibuni.
“Sexyyy record with a sexyass chocolate beauty! cant wait.. @vanessamdee x @shaydeeboi, #Tanzania #Nigeria,” ameandika msanii huyo kwenye kipande cha video alichokiweka kwenye mtandao wa Instagram.

Vanessa akiwa studio na msanii wa Nigeria Shaydee aliyemshirikisha kwenye wimbo wake
Naye Vanessa amepost picha akiwa na msanii huyo na kuandika, “Shaydee On The Single x Money on The Track … I’m calling S.O.S @shaydeeboi you a bad man, the FIRE THOUGH!”
Katika hatua nyingine Alhamis hii Vanessa Mdee ataungana na 2 Face na Iyanya kwenye show iliyopewa jina 2 Face and Friends Grand Party.

Categories: celebrity
0 comments:
Post a Comment