WASANII WA MUZIKI TANZANIA WAZIDI KUWA TISHIO KWENYE MTV NA TRACE TV, JAYDEE NAYE YUMO

Posted by Unknown on 17:05 with No comments
jide mtv
Wiki iliyopita baada ya video ya Joh Makini ‘Nusu Nusu’ kushika namba 1 kwenye chart ya video za wasanii wa Afrika ya MTV Base, na Diamond kukamata nafasi ya kwanza kwenye chart ya Trace Urban, mwanamuziki wa kike Lady Jay Dee pia ameingia kwenye orodha hiyo.
Video ya Jide ‘Give Me Love’ aliyowashirikisha wasanii wa Afrika Kusini, Uhuru, Mazet na Maphorisa, imeingia na kukamata nafasi ya 5 kwenye Official African Chart ya MTV Base wiki hii, huku Joh Makini akishuka kwa nafasi moja hadi nafasi ya pili.
Categories: