EFM yashinda tuzo za Tanzania Leadership 2015
Posted by Unknown on 16:58 with No comments

Kituo cha redio cha EFM cha Dar es Salaam, kimeshinda tuzo za Tanzania Leadership [Awards] zinazotolewa na taasisi maarufu ya Purple Cow.

Utoaji wa tuzo hizo ulifanyika Ijumaa iliyopita kwenye hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro. Katika kipengele cha Kituo Bora cha Redio mwaka 2015, nafasi ya pili ilikamatwa na TBC Taifa.
Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa EFM, Dennis Ssebo amesema ushindi huo una maana kubwa kwao.
“Sina wasiwasi kwa mafanikio haya kwasababu juhudi zetu zinajidhihirisha wazi na hatuna hata miaka miwili katika biashara hii lakini kwa kipindi hiki kifupi tumekuwa miongoni mwa redio bora na zenye wasikilizaji wengi jijini Dar Es Salaam, na hata kuvifanya vituo vingine Vikubwa na vikongwe vya radio kuvutiwa na aina ya utangazaji wetu. Hivyo, kwa mtazamo wangu mafanikio haya sio madogo.”
Categories: celebrity
0 comments:
Post a Comment