Hivi ndivyo Ajali ya New Force ilivyokuwa
Posted by Unknown on 08:20 with No comments


Basi la kampuni ya New Force baada ya kugongana na lori eneo la Igeme, wilayani Kilolo, Iringa leo mchana. Picha kwa hisani ya Michuzi blog
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi mkoani Iringa, basi la New Force lilikuwa linatokea jijini Dar es Salaam kuelekea Tunduma, mkoani Mbeya, na baada ya kugongana na gari hilo la mizigo, yalipinduka.
Jeshi la Polisi mkoani Iringa limethibisha kutokea ajali hiyo na kuongeza kuwa majeruhi wamewahishwa hospitali ya wilaya ya Kilolo huku wengine waliokuwa taabani wamekimbizwa hospitali ya mkoa wa Iringa.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Iringa, madereva wa basi na lori ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo na uchunguzi unaendelea.
Categories: NEWS
0 comments:
Post a Comment