Hizi ni sababu za wananchi wa Rwanda kumchagua Kagame

Posted by Unknown on 08:25 with No comments




 Rais wa Rwanda Paul Kagame amewaongoza wananchi wa taifa katika zoezi la upigaji kura ya maoni ili kubadilisha katiba iliyopo na kuandaa nyingine itakayomuwezesha kuendelea kuwa madarakani kwa muhula mwingine.
Kagame ambaye alipigia kura katika kituo cha shule ya Msingi Ape-Rugunga aliwasili kituoni hapo majira ya saa 5 na nusu akiwa ameambatana na mkewe na binti yake.
Baada ya kupiga kura Kagame aliwataka waandishi kutomuulizana chochote kwa sasa ila  atatao msimamo wake baada ya matokeo kutangazwa.
Kwingineko katika mji wa Kigali hali ya utulivu ilionekana kutawala kwenye maeneo mengi huku watu wakionekana kuwa na shauku ya kupata matokeo baada ya kupiga kura.
Mapema saa moja asubuhi vituo vilifunguliwa na watu walijitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya msingi huku wengi wao wakidai kuwa zoezi hilo ndilo litakaloamua mustakbali wa Rwanda.
Mmoja wa wananchi hao Charles Kaijamahe alisema Kagame ameiletea mafanikio makubwa nchi hiyo hivyo ana kila sababu ya kuendelea kubaki madarakani ili alete maendeleo zaidi.
“Kama unavyotuona leo Wanyarwanda tuna furaha hiyo yote ni kwa ajili ya Kagame amefanya mambo mengi mazuri ndiyo maana tunataka arejee ili azidi kutuletea maendeleo.
Wenyewe ndiyo tuliomba kipengele kinachomzuia Kagame kibadilishwe na hatimaye leo tunafikia hitimisho kwa kupiga kura hii yenye maana sana kwa taifa letu”alisema Kaijahamea.
Kwa upande wake Robert Ssali alisema kwa hatua iliyofikia Rwanda bado inamuhitaji Kagame ili aendelee kuivusha kwenye maendeleo.
“Tuna umoja na mshikamano wa kitaifa,demokrasia yetu iko vizuri ametuletea maendeleo,huduma bora za afya ni wazi kuwa huyu ndiye anayetufaa hivyo tunataka aendelee kutuongoza”alisema Ssali.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Rwanda  Profesa Kalisa Mbanda vituo zaidi ya 15000 vilitengwa kazi hiyo ili kuwapa fursa wanyarwanda kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
Profesa Mbanda alisema vituo vyote vitafungwa saa tisa na kufuatiwa na zoezi la uhesabuji kura ili  kuwezesha kutangazwa kwa matokeo ya awali ifikapo saa 11 jioni.

Categories: