Mazungumzo ya Raisi Magufuli na Seif yalikuwa hivi

Posted by Unknown on 11:23 with No comments



Image copyrightKwa Hisani
Image captionMagufuli akutana na Seif kujadili Zanzibar
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zanzibar-CUF Maalim Seif Hamad amefanya mazungumzo na rais John Magufuli wa Tanzania katika harakati za kujaribu kusuluhisha mzozo wa kisiasa unaokumba kisiwa hicho.
Mazungumzo hayo ya rais Magufuli na Seif Sharrif Hamad pia yalihudhuriwa na makamu wa rais bi Samia Suluhu Hassan.
Katika taarifa kutoka ikulu ya Dar es Salaam rais Magufuli alimshukuru Dr Ali Shein na Maalim Seif kwa jukumu la kutafuta amani kisiwani humo.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa upinzani wamekashifu mkutano huo na kusema kwamba mazungumzo yoyote kuhusu mzozo wa Zanzibar yafaa yawahuhishe viongozi wote.
Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha kijamii CCK Constantine Akitanda aliiambia BBCM kuwa upinzani ulipaswa kujumuishwa kwa pamoja kama washirika wa uchaguzi mkuu uliotibuka wa kisiwa cha Zanzibar.
Image copyrightZanzibar Electoral Commission
Image captionKisiwa cha hicho kilitumbukia katika mzozo wa kisiasa baada ya tume ya uchaguzi kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi
Akitanda alisema kuwa viongozi wakuu wa vyama vyote na tume kwa pamoja na rais wanapaswa kujadili mstakabal wa kisiwa hicho kisiasa.
'je watajadili wawili pekee yao ilhali wanapanga uchaguzi utakaotuhusisha sisi sote ?''
Haipaswi kuwa hivyo alisema Akitanda.
Kadhalika, kura zilidaiwa kuwa hazikupata ulinzi mzuri hususan kisiwani Pemba ambako baadhi ya mawakala wa vyama vya siasa katika kisiwa hicho walifukuzwa.
Vilevile vijana walidaiwa walivamia vituo vya kupigia kura kwa lengo la kutaka kuzua ghasia, na pia vyama vya siasa vilionekana "kuingilia majukumu ya tume ikiwemo kujitangazia ushindi na kupelekea mashindikizo kwa tume."
Categories: