Wanachuo kufaidika na mpango huu wa bodi ya mkopo

Posted by Unknown on 19:38 with No comments

Bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini imesema kwasasa imekwishaimarisha mifumo yake ya kupokea na kushuhulikia malalamiko ya wanafunzi haswa kwa waliokosa mikopo kwenye bodi hiyo.
Hayo yamebainiswa na meneja wa habari, elimu na mawasiliano wa bodi hiyo Bwana Omega Ngole huku akisema bodi hiyo kwasasa imejipanga vyema katika kuhakikisha wanafunzi wanaomba mikopo wanapata mikopo kwa wakati.
 
Bwana Omega Ngole ametoa wito kwa mafisa mikopo wa vyuo hapa nchini kuhakikisha wanabainisha matatizo ya wanavyuo na kuyashuhulikia kwa wakati ili kupunguza migogoro ya wanavyuo hao katika upatikanaji wa mikopo.
Categories: