
WAKATI muswada wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2016 ukitarajiwa kuanza kujadiliwa bungeni leo ambao unaoipa serikali mamlaka ya kisheria kutoza kodi na kutumia fedha hizo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, ametaja kodi ambazo zitalazimika kukatwa.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi kufafanua hoja ambazo hakuzielezea kwa kina bungeni, Dk Mpango alisema miongoni mwa kodi hizo ambazo baadhi ya wabunge na vyombo vya habari vilitetea...