INSPEKTA WA POLISI AANZA KUTOA USHAHIDI KATIKA KESI YA ALBINO, MWANZA
Posted by Unknown on 08:48 with No comments
SHAHIDI wa sita katika kesi ya mauaji ya Aaron Nongo mwenye
ulemavu wa ngozi (albino), Mkaguzi wa Polisi (Inspector) David Mhanaya, ameanza
kutoa ushahidi wake leo hii katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
Mbele ya Jaji Robert Makaramba anayesikiliza Shauri hilo
namba 213 la mwaka 2014, shahidi huyo ametumia siku nzima kutoa ushahidi wake
akiongozwa na mawakili wa serikali Emil Kiria, Esther Majaliwa na Robert
Kilando.
Hata hivyo, Jaji Makaramba aliahirisha kesi hiyo hadi
keshokutwa Mei 14, 2015 baada ya kutokea mgongano wa kisheria katika masuala ya
vidhibiti kufuatia pingamizi la Wakili Makwega wa upande wa utetezi, hivyo siku
hiyo atatoa uamuzi kuhusiana na pingamizi hilo.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Chacha Jeremia, Mathew
Jeremia Mlimi, Paschal Lugoye Mashiku na Alex Joseph maarufu kama Bugwema
Silola Jangalu.
Marehemu Nongo aliuawa Juni 26, 2009 majira ya saa tatu
usiku akiwa nyumbani kwake Ibanda Relini, jijini Mwanza ambapo wauaji hao
walimkata usoni na kisha kumkata miguu yake yote miwili na kutoweka nayo pamoja
na meno mawili ya mbele.
Categories: NEWS
0 comments:
Post a Comment