Tetemeko jipya Nepal laua watu 40
Posted by Unknown on 08:59 with No comments
- 12 Mei 2015
Wakati kukiripotiwa mvua kubwa na tetemeko kubwa na jipya
nchini Nepal, Wakuu nchini humo wamethibitisha kuwa idadi ya watu waliokufa
kutokana na tetemeko hilo jipya , imepanda na kufikia zaidi ya watu 40. Wakati
huo huo helkopta ya kikosi cha majini ya Marekani,ambayo ilikuwa ikifanya kazi
ya kusaidia kusambaza huduma za kibinaadamu nchini Nepal, haijulikani.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa, ndani ya helkopta hiyo
kulikuwa na watu nane,miongoni mwao, sita ni askari wa kikosi cha majini cha
Marekani na askari wawili wenyeji wa jeshi la Nepal.
Maofisa wa serikali wa Marekani wamesema kwamba helkopta
hiyo ilikuwa maeneo ya jirani na kijiji cha Charikot, ambacho kiliharibiwa
vibaya na tetemeko la ardhi.
Categories: NEWS
0 comments:
Post a Comment