Marekani kuishambulia Al-Shabab.

Posted by Unknown on 13:26 with No comments


MarekaniImage copyrightAFP
Image captionMarekani imesema wapiganaji zaidi ya 150 waliuawa
Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabab nchini Somalia limethibitisha kwamba maeneo yake yalishambuliwa kwa mabomu na Marekani.
Hata hivyo, kundi hilo limesema taarifa kwamba zaidi ya wanamgambo 150waliuawa kwenye mashambulio hayo yaliyotekelezwa na ndege zisizo na rubani “zimetiwa chumvi”.
Wizara ya ulinzi ya Marekani ilisema wapiganaji 150 wa al-Shabab waliuawa kwenye mashambulio yaliyotekelezwa Jumamosi katika kambi ya mazoezi ya wanamgambo hao.
“Marekani ilirusha mabomu katika eneo linalothibitiwa na al-Shabab. Lakini walitia chumvi kwenye idadi ya waliofariki. Hatuwezi kuwaweka pamoja wapiganaji 100 kwa sababu za kiusalama. Tunajua kumejaa ndege angani,” msemaji wa kundi hilo Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia Reuters.
Hata hivyo hakusema ni wapiganaji wangapi wa kundi hilo waliuawa.
Categories: