Majaliwa kusitisha mradi wa ECO ENERGY.
Posted by Unknown on 21:39 with No comments
Katibu wa Kamati ya HakiArdhi ya Bagamoyo (Bagamoyo Land Right Task Force), Jumanne Salumu amesema kwa niaba ya wananchi yao kuwa kabla ya kusitishwa mradi huo, Serikali ilipaswa iwashirikishe na kutoa maelekezo ya umikili wa ardhi hiyo unakuwa wa nani baada ya mradi kusitishwa.
Wamesema kitendo cha Serikali kusitisha mradi bila ya kuwashirikisha ni kuwaacha hewani na kuibua mgogoro.
Waziri Mkuu alitoa taarifa hiyo wakati akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Freeman Mboye alilouliza Mei 19 kutaka kujua sababu zinazosababisha Serikali kushindwa kuweka jitihada za makusudi katika kuhakikisha mradi huo wa miwa unatekelezwa kikamilifu kwa lengo la kupunguza au kuondoa tatizo la uhaba wa sukari nchini.
Katika majibu yake, Majaliwa alisema Serikali imeamua kusitisha mradi huo kwa sababu ungetumia sehemu kubwa ya maji ya Mto Wami hivyo kuathiri ustawi wa Hifadhi ya Saadan na wanyama wenyewe.
Categories: habari
0 comments:
Post a Comment