Chadema yafungua upya kesi

Posted by Unknown on 20:01 with No comments



Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.

Mwanza. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefungua upya kesi dhidi ya amri ya polisi ya kupiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa baada ya kuifanyia marekebisho hati ya awali ya mashtaka kwa kuwaondoa baadhi ya washtakiwa.
Mawakili wa Chadema Gasper Mwanaliela, John Mallya na Paul Kipeja waliwasilisha mahakamani hati mpya ya madai kwa kuondoa wadaiwa wawili ili kukidhi mahitaji ya kisheria.
Wadaiwa katika hati mpya ya mashtaka iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Awali, washtakiwa wengine walikuwa ni wakuu wa polisi Wilaya za Kahama, Maswa na Kamishina wa Operesheni na Mafunzo wa Polisi, Nsato Mssanzya

Categories: