mwenyekiti wa bodi TPA
Posted by Unknown on 20:03 with No comments
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amemteuwa Profesa Ignas Rubaratuka kuwa Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Profesa Rubaratuka ni Mhadhiri Mwanandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Atashikilia nafasi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu.
Akizungumza na vyombo vya habari leo Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Dk Leonard Chamuriho amesema Rais Magufuli amemtewa Profesa Rubaratuka kwa mujibu wa sheria namba 17 ya mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania.
Categories: habari
0 comments:
Post a Comment